TBS wanarudisha nyuma utoaji wa mizigo bandarini

ikipendaroho

JF-Expert Member
Jul 26, 2015
3,903
3,850
Wadau salamu zenu

Wakati mh Rais John Magufuli alipotoa maagizo kwamba wadau wote wanaohusiana na masuala ya bandari katika utowaji wa mizigo wafanye kazi kwa masaa 24 ili kuongeza uzalishaji na kupunguza usumbufu kwa wateja, TBS wao bado wanakwamisha zoezi hilo kwa kufanya kazi kwa masaa wanayotaka wao wenyewe.

Hivi nikiandika leo habari hii, wamefungua ofisi saa tano asubuhi huku wakijua kwamba benki wanazotumia ku deposit malipo yao wanafunga saa 7 mchana. Kuna benki nyengine ambazo zinatumiwa kufanya malipo kwa TRA na TPA zinafungwa saa 2 Usiku leo Jumamosi, wao TBS wameshindwa kutumia nafasi hii na kulazimisha wateja kulaza mzigo kwa siku za ziada na kwa maana hiyo kunyima wateja wengine kutumia nafasi bandarini ambayo ni useful limited resource.

Kiutaratibu, huwezi kutoa mzigo bandarini bila ya kupata TBS release certificate hata kama itakuwa umeshakamilisha hatua zote nyengine za utowaji mzigo bandarini. Udhaifu huu wa TBS unarudisha nyuma hatua za serikali za kuzidisha mapato ya Taifa kwa kuharakisha mzunguko wa malipo na utoaji wa mizigo bandarini.

Suala la kujiuliza, je hili linafanywa kwa makusudi kudhoofisha hatua za maendeleo za serikali au ni uzembe kwa maofisa wa TBS kwa kutokuwa na ubunifu na elimu ya kutosha juu ya suala zima la maendeleo ya Taifa hili?

Kuna haja ya kuliangalia hili suala kwa ukaribu sana kwa wadau wanaohusika.

Pamoja tuijenge nchi yetu!

======

UPDATE:

======

TBS watolea Ufafanuzi wa Malalamiko haya. Zaidi soma=> TBS yatolea ufafanuzi taarifa iliyotolewa Jamiiforums kuwa inadidimiza juhudi za Rais John Magufuli
 
Back
Top Bottom