Tbs,tfda na wizara ya afya ni uchochoro wa wababaishaji.

chikira

Member
Jul 25, 2008
21
0
Hawa wasomi walioko TBS(Tanzania Bureau of Standards),TFDA(Tanzania Food and Drugs Administration) na Wizara ya Afya sijui vipi.Miaka nenda miaka rudi tunaona bidhaa feki ikiwa ni vyakula,madawa,nguo nk.vikifurika nchini.Madawa feki na yaliyokwisha muda yamejaa kwenye maduka.Watu wanaendelea kufa hakuna anayejali.Mungu wangu,hivi ni nani atakaye tusaidia?Hawa wasomi ambao ndio tulidhani watatusaidia ndio wamekuwa mwiba.Sasa ni wasomi mamluki na uchwara, ambao wanashirikiana na wahasimu wetu kutumaliza.Watanzania tuamke,tusipoangalia tutakwisha.
 
TBS na TDFA ni makampuni ya uhalalishaji wa bidhaa feki. Wakishapokea ada na kugonga/kuidhinisha bidhaa iliyoletwa kama sample, huo ndio unakuwa mwisho wa uhakiki. Matokeo ya huu usanii ni kujazana kwa bidhaa feki zenye nembo zao - mikate yenye nembo lakini chini ya 500gm, peremende zenye ladha mbalimbali ndani ya mfuko mmoja, capsules zilizojazwa unga wa mhogo, chanjo zinazoleta madhara kwa watoto etc.
 
Kweli sijawahi kuona government institution zilizo hovyo kama hizi mbili, wao kazi yao ni semina na vikao tu! Pia kuna taasisi inaitwa BRELA...! Jamani hii taasisi ni chafu, mbaya, manual na imepitwa na wakati kuliko...!

Mi nashauri kama kama serikali haioni umuhimu wa taasisi hizi iwe inazifunga tu...! isipoteze muda kuzianzisha na kushindwa kuzipa uwezo...!
 
Back
Top Bottom