TBS! TBS!na NSSF tu? PPF ni ya CAG au ya Mkulo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBS! TBS!na NSSF tu? PPF ni ya CAG au ya Mkulo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mchukiaufisadi, Apr 20, 2012.

 1. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  TBS na NSSF vimetajwa mno kwa ubadhilifu lakini mbona sauti dhidi ya PPF hazionekani?

  Mikopo isiyolipika NSSF inafanana na ya PPF lakini ni NSSF ndio wanaonekana ni bata na PPF ni Kuku.

  1. PPF walimkopesha Dr Rshid mwenye Mikumi hospital, deni likafikia Bilioni moja na nusu ili kuwa na kiwanda cha maziwa kibaha. Alichokifanya ni kuitumia pesa hiyo kujenga hospital yake pale mikumi. PPF wakala hasara maana pale kibaha PPF iliambulia Tshs. Mil 45 tu out of 2Bilion

  2. PPF walimkopesha mfanyabiashara maarufu wa Shinyanga, Bw, Phantom, deni likafikia bilion 2, aliweka dhamana ya jengo la choo pale sinza karibu na Meeda Bar. Deni hili limefutwa baada ya wakurugenzi wa PPF kupewa chao kimyakimya na kuiconvise bodi ya fisadi Mgonja.

  3. PPF waliikopesha Kagera Sugar 7.5 Bilion, kama NSSF, lakini PPF watoto wa Mkulo na Utouh hawasemwi kabisa. Kagera Sugar walichukua Tshs 85Bilion kutoka mifuko ya pension na ni zaidi ya miaka 6 sasa hakuna malipo. Mwaka 2008, EL akiwa Waziri Mkuu aliagiza mifuko ifute riba ya karibu 20Bilion kwa Kagera Sugar baada ya yeye naye kupata chake. PPF mbona hawasemwi kwa uzito wa haya makosa? Hata Zitto anawaogopa

  4 PPF wanaskendo ya wakurugenzi kugawana kinyume na taratibu za mfuko na za fedha kila mmoja Tshs 220 Milion, na Tshs 520 Milion kwa Mkurugenzi Mkuu Bw William Erio, je Mkurugenzi wa TBS ameiba kama hizi? au hana mkubwa kama Mkapa wa kumtetea?

  5. PPF walikuwa na mradi mkubwa wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu Mwanza Kiseke, wameutelekeza, sasa Bw. Erio (DG) amehamishia raslimali kwao Mtwara. Ili kufanya mambo yawe rahisi amefungua ofisi ya Kanda huko na kumhamishia Meneja wa Morogoro ambaye ni rafiki yake mkuu. JE!!!!!!

  6. PPF wametumia pesa za watumishi wa Mtibwa Sugar, ambao ni vibarua walioondoka kabla ya kulipwa Tshs 25,000,000. Mtibwa Sugar walimwamini Meneja wa Kanda Bw. Meshack Bandawe wakampa awagawie wakija ofisi ya Morogoro badala ya wao kwenda Mtibwa. Meneja kazitafuna na DG alipoona hivyo akamhamishia Mwanza. JE!!!!!!

  Nita update mengine baadaye.

  Naomba Zitto, CAG na Mkulo watupe majibu.


  Source: mimi mwenyewe mfanyakazi wa PPF
   
 2. Shagiguku

  Shagiguku JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 400
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  sawa mfanyakazi wa PPF endelea kutupatia madudu na mauozo yaliyomo humo ndani mwenu. isipokuwa jaribu kuwa makini wasije wakaku-kanumba hao hao ma-director.
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  PPF sii inaongozwa na ndugu ya mkapa?na mtibwa na kagera sugar mali za mkapa hilo halina ubishi
   
 4. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Naona huyu hajui kilichowakuta wenzake...
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Mpatie hizo docs dr slaa na zitto!
   
 6. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Wewe si unajua interest walizo nazo? hawamtaki Dau full stop!
   
 7. mankipe

  mankipe Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kaka CAG hafanyi kazi kwa tetesi anafanya kwa evidence..km unayo iyo evidence na ukaidokeza kwa wakaguzi kipindi cha ukaguzi wangeifanyia kazi, unataka aseme kitu bila supporting document? afu mwisho mseme ana chuki binafsi? na ww umepata wapi huo ushaidi na usiupeleke TAKUKURU
   
 8. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kesi ya shamba la mifugo la Kibaha na ya Phantom ilikuwa mwaka 1997 na iliandikwa na gazeti la Rai kutokea Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambako wote walishitakiwa na PPF kwa kushindwa kulipa hizo fedha. Sasa kama ni ya mwaka 1997 Erio hapa anatokea wapi? Hizi mada zinaanza kurudi tena. CAG wa sasa pamoja na matatizo yake, anafanya kazi kwa umakini zaidi na ndiye anayesababisha haya mambo yote kutokea sasa, kwa hiyo kusema CAG hafai kwa kuwa hajawafurahisha wabaya wa Erio haina maana kabisa.
   
 9. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Huyu ni kiongozi wa kamati ya mahesabu ya mashirika ya umma..inabidi awe anafahamu kinachoendelea ppf King Kong III
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Mkopo ulitolewa 1997, wakati wa Davidi Mattaka, hilo halina ubishi. Erio ndio kafuta deni. Usimtetee huyu wewe humjui.

  Siogopi kufukuzwa kazi kama alivyowaonea wale mameneja ili awape ajira ya ajira wapenzi wake. Hata yeye sio wa kudumu atafika muda wa kuondoka ambao Mungu anaujua ataondoka. Nichukiacho mimi ni udokozi wa mali za umma. Mbona hujabisha kama alivuta Tshs 520 milioni za Group Endowment wakati hastahili?
   
 11. nxon

  nxon JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,149
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  ina kera kinoma
   
 12. T

  The Eagle Member

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkaguzi anapofanya kazi yake anapaswa kuona haya madudu na sio kupelekewa kwani yeye co polisi au mahakama wanaothibitisha hatia ya mtu. Inamaana CAG hakufika PPF au huu ni uzushi au nayeye alipewa chake?NAWAZA TU.
   
 13. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kuna kiongozi mmoja alipata kusema kuwa huu ni upepo tu wa siasa utapita..
   
Loading...