TBS na TRA mpo wapi kuwakinga Watanzania na hii kampuni ya KC Global Link?

hotstoryg

Member
Apr 16, 2011
16
8
Hii kampuni imekuwa ikiingiza mizigo/makinikia toka UK, cha ajabu vitu wanavyoviingiza kama used ni vibovu sana na asilimia 60 vinakuwa huwezi kuvitumia mpaka uwatafute mafundi huku yeye akiendelea kunadisha mnada ambao unafanyikaga online kila wiki na ofisini kwao mikocheni nyuma ya clouds.

Je, TBS kazi yao ni kuangalia ubora wa vitu kama magari tu na vyakula? Je wananchi wanaoletewa mizigo used toka ulaya hawana budi kukingwa na huu utapeli unaofanyika.

Pili ukinunua vitu kwao ukienda kulipia wanakupa lisiti ya TRA ambayo wameipunguza bei tofauti na uhalisia, TRA fuatilie mahesabu ya hii kampuni na bei anazouza ktk minada anayofanya tokea facebook kuna ukwepajinmkubwa sana wa kodi na ata vitu anavyouza ofisini kwao mikocheni mtagundua udanganyifu mkubwa sana wa kodi toka katika hii kampuni.

Mimi mmojawapo ni muathilika wa hili na ushaidi wa receipt niliyopewa ikiwa imepunguzwa bei halisi niliyonunulia vitu ninayo, na hata clip ya video inayoonesha bei halisi ya kununua hivyo vitu ninayo mkianzisha uchunguzi nitatoa ushirikiano.


Naambatanisha picha kuthibitisha ubovu wa bidhaa zao na lugha zao wanazotumia kuhalalisha ubovu wa vitu huku wakiwa hawana wasi wasi kuingiza vitu bibovu nchini

IMG_2351.jpg


IMG_2350.jpg

IMG_2349.jpg

IMG_2348.jpg

IMG_2347.jpg

IMG_2346.jpg

IMG_2345.jpg
 

Attachments

  • IMG_2351.jpg
    IMG_2351.jpg
    137.4 KB · Views: 7
  • IMG_2350.jpg
    IMG_2350.jpg
    150.4 KB · Views: 10
Hahahahahahahahahahahahaha.........
Kwahiyo mkuu hivyo vya kwenye picha ndio.vipo mnadani au umeamua kuwachafua tu!!

Watu wa vyuma chakavu hivyo vinawafaa sana.

Hivyo ndio vipo wameuza jana. Ndio maana unaona na namba yao wanayotumia kutangaza
 
Nadhani muhusika hapo si TRA, bali TBS ndio wanapaswa kuulizwa kama wameruhusu import ya vyuma chakavu.

TRA iangalie udsnganyifu wanaofanya wa kuandika recept ambayo wanashusha bei halisi ya pesa iliyolipwa na mteja na mm ni muhanga wa hilo mkuu
 
Mi nafikiri tangazo lao limejitosheleza,Tena na wamekupa tahadhari kabisaaaa.
Tatzo Ni sisi tunapenda kua na kitu kutoka ulaya kwa bei kitonga.
Mbona michina imejaa kibao tu na bei rahisi japo wajua after one or two year's Haina kaziii?

Cheap Ni gharama Sana mkuu,beba tu vyuma vyako katengeneze na upake na rangi hasa pale palipoandikwa MADE IN UK ili uturingishie unatumia kitu OG
 
Hii biashara ya kuuza vitu used nimemuzia sana ndg yangu mmoja yuko anaishi denmark alikuwa akileta bongo mafriji,majiko,baiskeli,vyombo vya ndani bidhaa kibao na ktk bidhaa hizo watu walikuwa wakija hawachomoki kutokana na ubora wa vitu
Siku ya kufungua kontena watu saa 12 kamili wapo nyumbani njeee
Ila tu kwwnye kuuza kulikuwa na bei ya test na no tested ya vitu vya umeme
Ila kasoro ndg ndg zolikuwa hazikosi...
Bidhaa toka scandnavia countries ni nzr sana

Ila hao jamaa hapo wametisha

Ova
 
Mkuu, kwani unalazimishwa kununua?
Mkuu Kwa uelewa wako ni kuwa mtu hata akiuziwa vitu vilivyoisha muda wake hapaswi kulalamika maana hajalazimishwa.

Wajibu Wa serikali ni kuwalinda wananchi wake,tukisema kuwa mtu hajalazimishwa tutakuwa tunahalalisha wizi na utapeli
 
Mkuu , hivi vitu ni nani ananunua? Na wanauza bei gani na mbna kama hayo ni ma screpa tu?? Kuna mtu mwenye akili timamu kweli ananunua vitu kama hvyo?

Mkuu watanzania wengi wakishasimia vitu vinetoka uingereza basi wanapapatika bila kuelewa... yaani ukiongea kutetea kama hivi wanakushambulia sana. Hii imempa jamaa chriss lukosi kiburi kupita kiasi hadi anafikia kuwadhiaki wateja wake kwa maneno ya kejeli sana. Wakati wapo watu wengine wanatoa vitu huko UK na sehemu nyingineza ulaya ila ubora unakuwa mkubwa mno. Sasa ni wakati wa serikali kutusaidia
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom