TBS na TRA mpo wapi kuwakinga Watanzania na hii kampuni ya KC Global Link?

Anafanya biashara ya vitu used analipa kodi ya serikali ameajiri watanzania pale mikocheni B
Anauza mpka magari used nimewahi nunua kifaa kwake sijahangaika kwa fundi mpka leo
Vitu vizuri anavyo vingi tu sema wewe cjui ulienda kufuata screpa na namna gani maana anazo kila aina ya used iliotumika siku moja mpa miaka kadhaa
 
Eeehh haya matakataka yamepita Bandari yetu ya Dar kweli? Eeehh hizi si rust au kutu tupu.. Kweli TBS mko wapi? Eeeh, hapa TBS lazima watatumbuliwa.
Hapa FCC inatakiwa ifanye jukumu lake
 
Mkuu , hivi vitu ni nani ananunua? Na wanauza bei gani na mbna kama hayo ni ma screpa tu?? Kuna mtu mwenye akili timamu kweli ananunua vitu kama hvyo?
Huyu Hana kitu kichwani, hayo maskrepa ndo analalamika kanunua vitu used?
 
Hii kampuni imekuwa ikiingiza mizigo/makinikia toka UK, cha ajabu vitu wanavyoviingiza kama used ni vibovu sana na asilimia 60 vinakuwa huwezi kuvitumia mpaka uwatafute mafundi huku yeye akiendelea kunadisha mnada ambao unafanyikaga online kila wiki na ofisini kwao mikocheni nyuma ya clouds.

Je, TBS kazi yao ni kuangalia ubora wa vitu kama magari tu na vyakula? Je wananchi wanaoletewa mizigo used toka ulaya hawana budi kukingwa na huu utapeli unaofanyika.

Pili ukinunua vitu kwao ukienda kulipia wanakupa lisiti ya TRA ambayo wameipunguza bei tofauti na uhalisia, TRA fuatilie mahesabu ya hii kampuni na bei anazouza ktk minada anayofanya tokea facebook kuna ukwepajinmkubwa sana wa kodi na ata vitu anavyouza ofisini kwao mikocheni mtagundua udanganyifu mkubwa sana wa kodi toka katika hii kampuni.

Mimi mmojawapo ni muathilika wa hili na ushaidi wa receipt niliyopewa ikiwa imepunguzwa bei halisi niliyonunulia vitu ninayo, na hata clip ya video inayoonesha bei halisi ya kununua hivyo vitu ninayo mkianzisha uchunguzi nitatoa ushirikiano.


Naambatanisha picha kuthibitisha ubovu wa bidhaa zao na lugha zao wanazotumia kuhalalisha ubovu wa vitu huku wakiwa hawana wasi wasi kuingiza vitu bibovu nchini

View attachment 1724436

View attachment 1724437
View attachment 1724438
View attachment 1724439
View attachment 1724440
View attachment 1724441
View attachment 1724442
Huyu atakuwa na tenda ya kuzoa taka na kuja kuzitupa tanzania
 
Back
Top Bottom