sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,487
Ingekuwa inawezekana kutukana ningeanza na matusi kabisa ili ujumbe ufike vizuri kwa wahusika.
TBS na TFDA ni majipu makubwa kuliko majipu yote tunayoyajua na utumbuaji wa majipu haya inafaa ipendekezwe njia ya kuyatumbua kama ambavyo tunaripoti wahalifu kama wezi polisi. Hizi taasis ndizo zimeshikilia AFYA za watanzania ila vitu feki ni vingi kupita maelezo na wao wakikurupuka wakipita, kukagua ni mara chache sana na hivyo kufanya bidhaa feki kuzagaa na kuingizwa nchini kwa wingi maana hamna hatu kali zinachukuliwa.
Baadhi ya bidhaa feki zilizokithiri na ambazo huenda zimesababisha madhara mengi kwa watumiaji kwakuwa kuzitambua si rahisi, na hata ukizitambua huna cha kufanya ni hizi:
¤Sukari
¤Mafuta ya kupikia
¤Vipodozi
¤Nyembe hadi zilizotumika
Mafuta ya kula ndo balaa zaidi Hivi mwuaji wa silaha ana tofauti gani na huyu anayekuua kwa kutumia vyakula? Mamlaka zinazofanya ukaguzi wa bidhaa za aina hizi zinapaswa kuweka sheria hata ya kunyongwa kwa hawa wauzaji wa bidhaa feki. Ni wauwaji. Wiki ijayo kuna simu zinafungiwa kwakuwa ni feki, ila wakati zinaingia ziliruhusiwa kutumika humu nchini na zitakuwa zimeshadhuru wengi!