TBS na TFDA, mmesikia Kenya walivyofungia unga wa mahindi?

Tuwekee utafiti unaothibtisha vyakula vya jamii ya kunde kama maharage ya soya uliyotaja, ukiachilia mbali karanga yanaweza kuwa na viwango vikubwa vya aflatoxin. Msiwe mnaweka vitu vya kuwapotosha watu humu ili mradi mwonekane na nyie mmechangia.
Maharage kama yana sumu basi mimi ndio ntafia hapo hapo!!!
 
Kenya wameshafunguliwa baaba ya kufanya utafidi viwanda vinavyosaga nafaka. Je Tanzania ina mpango gani kuvikagua viwanda vinavyosaga nafaka? Kwa kupitia TFDA na TBS?
TFDA ishakufa mzee watu wenye mikono mirefu walisha iua wamewaa TBS kazi ya chakula na vipodozi ambao hawajui waanzie wapi watanzania tunakufa kidogo kidogo na serikali ipo bize na uchafuzi wa mitaa
 
Una hoja nzuri sana, binafsi huwa nashangaa sana unakuta taasisi fulani moja wapo wa majukumu yao ni kuzunguka katika viwanda vya chakula na dawa lakni hawafanyi hivyo kutwa kukaa ofisini wanakula viyoyozi tu wakati watanzania wanateseka kwa kupata kansa inayosababishwa na nafaka tunazozitumia kama chakula.

Bado naona watanzania hawana elimu ya kutosha kuhusiana na food intoxication, hiyo sumu ya aflatoxin ni miongoni mwa sumu mbaya sana sema tu ndio hivyo, semina za uelimishaji hakuna kwa wananchi.
TFDA ishakufa mzee watu wenye mikono mirefu walisha iua wamewaa TBS kazi ya chakula na vipodozi ambao hawajui waanzie wapi watanzania tunakufa kidogo kidogo na serikali ipo bize na uchafuzi wa mitaa
 
Sumu ya Aflatoxin inayoweza kusababisha saratani ya ini, hupatikana kwenye mazao yaliyopata fungus na si kwa sababu ya dawa iliyopulizwa. Mazao kama karanga, mahindi, mihogo au hata mikate, isipotunzwa vizuri huanza kuota fungus/kuoza na fungus hao ndiyo hutoa hiyo sumu. Kuwa makini unapokula karanga mikoa ya dodoma na singida ambayo imeathirika sana, ambapo ukiona punje ya kwanza au pili ya karanga imeoza, bora usiendelee kuzila. Unakumbuka vifo kadhaa vya familia moja dodoma vilivyotokea baada ya kula ugali???
Mara nyingi husababishwa na hali ambapo nafaka zikisha komaa,hukosa jua LA kutosha kisha kuingiliwa na fungus
 
Back
Top Bottom