TBS na TCRA mmeruhusu wizi, watu wamepata hasara

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana JF,

Katika serikali makini TBS na TCRA wametuangusha sana kwa kuruhusu wizi wa kichina.

Anavyokuwa: watu ambao hawana fani yeyote ya ufundi, wamevamia mitaa na kulaghai watumiaji wa smart phone kuwa wanatengeneza kioo cha simu kwa kuweka liquid ambayo inakifanya kiwe imara, kwamba hakitaweza kuvunjika kwa urahisi. Wana machine za kutoboa vitu, wanawaonyesha kuwa kitu cha ncha kali hakiwezi kutoboa.

Kumbe in uongo mtupu, tena ni bahati mbaya sana hiyo dawa inayotumika ina kemikali kali sana ambayo haifai kwa matumizi ya binaddamu. Hicho kioo cha juu (touch screen) inakakamazwa tu hakuna uimara wowote.

Baada ya muda ikiguswa inavunjika vibaya full screen hakifanyi kazi tena, ambayo kama wasingeweka hiyo dawa ya mangumashi, ungeweza kuendelea kutachi hata kama kimevunjika vipande vipande kiasi cha kushindwa kuona vizuri.

Serikali kupitia vyombo hivi inalaumiwa kwa kuacha matapeli wasio na leseni kuendelea kuwaibia wananchi kwa udanganyifu huu.

Natoa rai kwamba, biashara za kitaalum inabidi TBS na TCRA waithibitishe ndio irihusiwe sio watu wanajibanza ukutani serikali haipokei chochote halafu watu wanaibiwa na wanaharibiwa vyombo vyao.

Touch inaweza kubadilisha kwa gharama nafuu, wakishaweka dawa hizi lazima uingie gharama ya kununua full screen badala ungenunua touch tu.
 
Serikali haiwezi kukulinda dhidi ya kila kitu, ndio maana unapewa elimu ya msingi bure ikusaidie kuyamudu mazingira yako, kama hiyo imeshindwa kukusaidia basi wewe unastahili kuibiwa.
 
Asante, nilikuwa naona nikasema ngoja kwanza mtangulie nisubiri mrejesho kama hivi.
Kinachofanyika hiyo liquid inapenya kwwnye layer ya touch na LCD/LED kukifanya kioo cha mbele touch kikakamae kwa muda Fulani kama mwezi mmoja hivibbaadae uisha nguvu na kioo uanza kupasuka maxima . uwezi kurepair layer ya juu mpaka ununue full kioo ambavyo kama no Samsung na Huawei, iPhone being take lazima utajuta kuwajua.
 
Kinachofanyika hiyo liquid inapenya kwwnye layer ya touch na LCD/LED kukifanya kioo cha mbele touch kikakamae kwa muda Fulani kama mwezi mmoja hivibbaadae uisha nguvu na kioo uanza kupasuka maxima . uwezi kurepair layer ya juu mpaka ununue full kioo ambavyo kama no Samsung na Huawei, iPhone being take lazima utajuta kuwajua.
Yaani inakuwa kama unaongeza unene wa kioo cha simu yako? Na mbaya huwezi tena kuja kutenganisha.
 
...hv hakuna ata mtu mwenye lile tangazo lao la liquid...tuusindikize huu uzi, ahahaaa

Kuna ule wimbo wa professor J,Bongo dar es Salaam....hii ndo bongo unauziwa cheni bandia kwa noti bandia.
 
Kuna mshenzi aliniijia nikiwa kiwanja kimoja Uyole Mbeya, kanishawisshi kweli akiwa na kiji-briefcase chake cha silver nikachomoa, kumbe ndo hao!
 
Duuu, watu washaa jenga nyumba na kutajirika tayr, wameuza sana hii bidhaa.
 
Kama umepigwa changa la macho la liquid protector hiyo ni police case hata TCRA hawahusiki hapo
Wanahusika kwa kuwa wanaooendesha biashara hii hawajapitia mafunzo yoyote ya kiufundi hivyo hawaruhusiwi kushika Mali ya mteja. Na hawa watu wanafanyabuaribifu kubwa kwa kuwa hawana makazi maalum na hawatoi tist ambavyo kama kuna mafhara uweze kuwashitaki
 
Back
Top Bottom