TBS na Bidhaa Feki Ongezeko la Kushuka kwa thamani ya Tsh

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
kumekuwa na wimbi la bidhaa nyingi feki, zenye waranty ya mwezi mmoja mpaka mitatu, bidhaa hizi hutufanya kununua au kuagiza vifaa mara kwa mara kutoka nje, jambo ambalo hutumika pesa nyingi kubadilisha dola. Nikifuatilia kwa karibu sana kuna bidhaa, kama vile pasi, redio, madishi, feni, taa, na vifaa vingi vya kuchezea watoto kama matoy ya gari.
Mtalaam mmoja wa uchumi kutoka Swede, alishangaa sana kuona tanzania tunatumia pesa nyingi kunulia madoli ya watoto, Pumpurs, vijiti vya kutolea nyama (vichokonoleo) wembe na sindano, akahoji kukosa viwanda vidogo kukabiliana na vitu hivi. Wabunge mfukuzeni mtalaamu huyu wa TBS anaye ruhusu simu za mchina zinazodumu mwezi mmoja ambazo huagizwa na kuuzwa kwa pesa nyingi. Vijana sasa hivi wameamua kurudia kuvaa ndala za kutumia magurudumu ya gari piki2,. Huyu jamaa hafai anashindwa hata kufika kariakoo akajionea adapter zilizoandikwa Made from Britain ambazo huyeyuka na kusababisha ajari ya moto, nina hasira naishia hapo.
 
Sasa tufanyeje mkubwa!? maana mengi tumeshayaongelea hapa ..................... action pls!!!
 
Sasa tufanyeje mkubwa!? maana mengi tumeshayaongelea hapa ..................... action pls!!!

dawa kuwaondoa wote na kutafuta jina lingine na kuzindua upya kama vile tulivyoiua FAT ya Rage na yule Mpayukaji
 
Back
Top Bottom