TBS Kamilisheni marekebisho ya Website yenu Mnakwamisha Mizigo Bandarini

Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,768
2,000
Tangu Alhamisi iliyopita TBS wanarekebisha website yao.

Kutokana na marekebisho hayo, huduma muhimu za kulipia Malipo ya TBS kwa magari yaliyo bandarini zimekwama. Mteja huwezi kutengeneza control number, hivyo huwezi kulipa, na hivyo mzigo hauwezi kutoka bandarini kwa sababu hiyo tu.

Kwa kampuni inayosimamia viwango, mkwamo huo ni mbaya sana kiuchumi.

Kadri mnavyochelewa ndivyo mnavyotia hasara wenye mizigo, kwa kuongeza tozo za bandarini.

Tunaomba mshughulikie hili haraka ili kunusuru shuguli muhimu za watu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom