TBL yapigwa faini kuvuruga ushindani wa kibiashara

Kabewa

Senior Member
Oct 30, 2009
136
56
KAMPUNI ya bia ya Tanzania Breweries Limited [TBL] imepigwa faini ya shilingi bilioni 518 kwa kukiuka na kuvuruga ushindani wa kibiashara nchiniHatua hiyo imechukuliwa na Tume ya Ushindani ya biashara [FCC] baada ya Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries [SBL] kulalamikia vitendo vinavyochukuliwa na kampuni hiyo shindani.

Hayo yamekuja baada ya TBL kukiuka misingi ya kibiashara kwa kungo'a mabango ya biashara ya kampuni ya SBL katika baa mbalimbali yaliyowekwa na kampuni hiyo kitendo ambacho si halali kwa kanuni za kibiashara nchini.

Mbali na hilo pia TBL imekuwa ikizuia kabisa bia za kampuni hiyo zisiuzwe na kuwaagiza wamiliki wa baa wasiuze bia za kampuni hiyo ya Serengeti.

Hivyo kutokana na vitendo hivyo adhabu kali imechukuliwa didi yao na tume hiyo imetoa adhabu ya kuwakata asilimia tano ya mapato ya mwaka mzima kutoka katika kampouni hiyo
source nifahamishe.com
 
wakome kabisa wamezidi kujitamba na kusupport kila kitu TZ TBL yenyewe ni ya wathungu hebu waoondoeni hao.
 
KAMPUNI ya bia ya Tanzania Breweries Limited [TBL] imepigwa faini ya shilingi bilioni 518 kwa kukiuka na kuvuruga ushindani wa kibiashara nchiniHatua hiyo imechukuliwa na Tume ya Ushindani ya biashara [FCC] baada ya Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries [SBL] kulalamikia vitendo vinavyochukuliwa na kampuni hiyo shindani.

Hayo yamekuja baada ya TBL kukiuka misingi ya kibiashara kwa kungo'a mabango ya biashara ya kampuni ya SBL katika baa mbalimbali yaliyowekwa na kampuni hiyo kitendo ambacho si halali kwa kanuni za kibiashara nchini.

Mbali na hilo pia TBL imekuwa ikizuia kabisa bia za kampuni hiyo zisiuzwe na kuwaagiza wamiliki wa baa wasiuze bia za kampuni hiyo ya Serengeti.

Hivyo kutokana na vitendo hivyo adhabu kali imechukuliwa didi yao na tume hiyo imetoa adhabu ya kuwakata asilimia tano ya mapato ya mwaka mzima kutoka katika kampouni hiyo
Wangeenda hadi COKE na PEPSI maana kuna maeneo (kwa mfano UBALOZI) sehemu moja kuna viti vya Coke (huuza soda jamii ya coke tu) na nyingine vya Pepsi (huuza soda za jamii ya pepsi tu).
 
Business Exclusivity or Exclusivity contracts contravene the FCC rules.
 
Hii ni ya siku nyingi na hiyo tume ikadai wao ndiyo walipwe na sio serengeti walioingia hasara.....kweli the law is blind...yaani muamuzi ndo alipwe ilhali mimi niliye shitaki kwa hasara nikipewa maneno matamu ya kisheria
 
Back
Top Bottom