TBC1 Wizi mtupu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBC1 Wizi mtupu!

Discussion in 'Entertainment' started by Kabota, Oct 21, 2009.

 1. Kabota

  Kabota Member

  #1
  Oct 21, 2009
  Joined: Aug 15, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15

  Jumamosi iliyopita nilikuwa naangalia concert ya MTV AFRICA MUSIC AWARDS iliyofanyika jijini Nairobi, Kenya kupitia kituo cha TBC1. Dah! kiukweli lilikuwa bonge la show kutokana na maandalizi ya wazee wa burudani, MTV pamoja na wasanii waliokuwa wakitumbuiza siku hiyo. Mwishoni kabisa yalitokea maneno 'PRODUCED BY BAZO TBC1" jambo lililonifanya nijiulize maswali kuwa huyo Bazo kaproduce nini hapo!

  Ile kukatakata sehemu mbalimbali kupunguza muda wa tukio lenyewe uwe katika muda uliopangwa na TBC kurusha concert hilo ndo kaproduce! Kwanza transition alizokuwa anaweka zilikuwa hovyo hovyo tu na kufanya matukio yasioane.

  Jamaa wa MTV wamekuja na crew ya watu kibao ikiwa pamoja na maproducer wa show nzima na kutoa kitu kama kile halafu mchizi anaiubuka tu from nowhere nakuandika show kaproduce yeye! Kiukweli kama MTV wakiona show yao imeandikwa imekuwa produced na Bazo haki ya Mungu lazima wamind kinoma!

  Bazo angejua jinsi shughuli ilivyongumu kuproduce show kama hiyo hata asingethubutu kuchukua credits toka kwa wazungu waliofunga safari toka Marekani kuja Kenya kwenye show hiyo.
  Kwanini show isiandikwe courtesy of MTV kuliko kuandika produced by Bazo wakati mzee hata hakutia maguu Nairobi? Sanuka mtu mzima! Ni hayo tu.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  aaaghhhhhh
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,152
  Trophy Points: 280
  Bazo ama zoba?
   
Loading...