Elections 2010 TBC1 waupa mgongo uchaguzi wa Igunga

mikatabafeki

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
12,772
4,641
nimekua nikifuatilia uchaguzi wa Igunga kwenye televisheni mbalimbali toka asubuhi lakini cha kushangaza ile tunayoifahamu kama televisheni ya Taifa ndo kwaanza haitoi hata updates ya kinachoendela huko

je matokeo ya vituo mbalimbali yanayotangazwa ndo yanawakatisha tamaa kutangaza habari za uchaguzi huu mdogo huko Igunga???

Je kaka mkubwa kule Ikulu kapiga biti kutoa updates za uchaguzi???


 
watangaze wakati wanaona wanafirigiswa chini. Uhuru fm wao wanadai ccm inaongoza kata 13 matokeo wamepata wapi?
 
TBC1 mizengwe kibao lakini ina mwisho wacha waana wa Tanzania wapambane .Changes zinakuja na wao watajuta .
 
TBC siiamini kabisa hasa yanapokuja maswala mazito kama haya! achana nao,tuangalie tu namna gani tutanusuru kodi zetu wanazolamba kujiendesha
 
wameona upepo mbaya kwa ccm ndo maana wameamua kua kimya. Wafuate mfano wa star tv walioendelea kurusha matangazo wakati bosi wao diallo akigaragazwa kule ilemela.
 
yaani wapo buz na kuonyesha miziki ya taarab utadhani hakuna jambo kubwa la kitaifa linaloendelea mwisho wa siku wanakuja kupewa tuzo ya coverage za uchaguzi wa Igunga,aaaha haaaa haaaa
 
TBC walikatisha matangazo ya igunga tangu asubuhi na wakaendelea na taarab na mambo mengi. Hii TV kweli ni aibu kubwa sana tangu aondoke Tido Mhando< Mkurugenzi mpya Daniel Mshana amekuwa ni muoga kupita kiasi wakati yeye mwenyewe yuko Igunga!!!
 
Back
Top Bottom