Tbc1 naomba mtofautishe matangazo ya moja kwa moja na dondoo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tbc1 naomba mtofautishe matangazo ya moja kwa moja na dondoo.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kichenchele, Jun 3, 2011.

 1. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 521
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Jamani ndugu zangu wa Tbc1 ukweli mnanikera sana pale mnapotangaza kwamba mtarusha matangazo ya michezo inayokuwa inafanyika nje ya nchi yetu, mathalani mpira na michezo mingine, lakini badala yake mnaanza kutoa maneno ya kumradhi n.k, mfano ilikuwa ni mechi ya TP-Mazembe na Simba ambapo mlionyesha kipindi cha kwanza tu na baada ya hapo mkasema mnaomba radhi kwa kukatika kwa matangazo hayo, juzi nikiwa nasikiliza matangazo ya mechi ya simba na Wydad Cassablanca, kupitia TBC-FM kipindi cha pili mkapotea na kuanza kusema kumradhi na mkawa mnapiga miziki ya akina marijan Rajab, Mbaraka mwishehe na kadhalika, na mkasema tutakuwa tunawaletea yanayojili huko, sasa mimi ningeomba mjaribu kuboresha vyombo vyenu vya kunasia matangazo au mtueleze ya kwamba mtakuwa mnatoa dondoo za matukio yanayotokea ktk eneo husika kuliko kumkalisha mtu anasubili matangazo ya moja kwa moja kumbe ni zimamoto,
   
Loading...