Tbc1 inajitahidi

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
TBC1 inajitahidi kutoa habari zenye uchambuzi wa kina.
Pia vipindi vyake vingi ni vya kuelimisha jamii,.
Kadhalika TBC1 imepunguza sana masuala ya udaku.
Izidi kufanya mabadiliko kwenye itikadi za kisiasa.
 
nafikiri hayo ni maoni yako. mimi binafsi huangalia TBC1 kukiwa na mpira au baadhi ya siku tamthilia lakini taarifa ya habari najiendea zangu ITV au star maana TBC wako biased. kwangu mimi ITV na star ni bora kuliko TBC1. anyway television ya taifa lakini ni watu wangapi tanzania wanayoiona ? Star TV kwa sasa inaonekana karibu tanzania nzima. Namaanisha hata watu wa kawaida ni kununua tu ka antenna (sio dish) na unaiona star. TBC1 no no.
 
Johnj:
Nadhani anachosema Exaud ni kulinganisha walipo sasa na TBC1 ilikotokea. Ni kweli kwamba ukitaka kitu kizima lazima uzichanganye mativiii yoooote ya bongo. Lakini TBC1 wamepiga hatua sana kulinganisha na walikotoka, wameweza kupata mechi za mipira yenye sifa sana duniani, wamejiunga na DStv, taarifa zao ni za ukweli kiasi na nadhani ndiyo tiiviii pekee kwasasa hapa bongo inayotoa taarifa ya habari "live". Labda nimpe sifa hizi Mheshimiwa Tido. Kwa upande wa taarifa za siasa bado wanalalia sasa "nyinyiemu" ni hiki ni "weakness" kwao.
 
Star TV ina watangazaji wasiojua kutamka majina kama Andy Murray( hadi hivi karibuni walikuwa wakitamka (Andi Mulei) na wakitangaza hawajiamini wnakuwa kama wamesimamiwa na kamanda hapo pembeni.Sura zao hazina ile bashasha ya kuwa huru kama wenzao wa TBC 1.

Star Tv wanakuwa kama wameganda...ningependa wajiendeleze katika taaluma na wasiwekewe vikwazo na wamiliki.Nataka wawe free kama vile wa CNN na TBC 1 kwa sasa.

Majina ya vipindi kama The Big Top Ten hayana mantiki kwa sababu ukishatamka TOP sasa BIG ya nini ...na kipindi hakitakiwi kiwe na maneno mengi maana unakuwa unachanganya habari za muziki na TOP TEN!Hata hivyo uzuri wa kipindi ni kwamba kinatoa nyimbo bora za Kitanzania tu...hapo Big up.

Katika vipindi vya komedi hawa wa TBC 1 hawana lolote la maana mtindo ule ule na comedians wanakuwa wanachosha.

Hawa wa Star TV ni wazuri ila hawana direction.

katika habari ni TBC 1 amabao japo ni TV ya Serikali lakini imeondokana na upendeleo wa wazi na sasa imejirekebisha na kutangaza bila bias.

Kwa ujumla stesheni zetu za Tv zinatakiwa kuboresha vipindi na kuwapa watazamaji habari za uhakika na burudani ya maana.
 
nafikiri hayo ni maoni yako. mimi binafsi huangalia TBC1 kukiwa na mpira au baadhi ya siku tamthilia lakini taarifa ya habari najiendea zangu ITV au star maana TBC wako biased. kwangu mimi ITV na star ni bora kuliko TBC1. anyway television ya taifa lakini ni watu wangapi tanzania wanayoiona ? Star TV kwa sasa inaonekana karibu tanzania nzima. Namaanisha hata watu wa kawaida ni kununua tu ka antenna (sio dish) na unaiona star. TBC1 no no.


Muzee wewe kama mimi ..
 
Star TV ina watangazaji wasiojua kutamka majina kama Andy Murray( hadi hivi karibuni walikuwa wakitamka (Andi Mulei)

Mie si walaumu sana kwa hili . Majina mengine ya kizungu ni magumu kutamka hasa kwa ndimi zilizozoea kiswahili. Hata watangazaji wa BBC (English) nao huwa wanachemsha kutamka majina ya kiafrika: Kwa mfano 'Mkapa' utasikia wanasema 'Makapa' nk. Hata hivyo kama kioo cha jamii wanapaswa kujiandaa kabla.

The rest of your criticisms are true and fair.
 
Mie si walaumu sana kwa hili . Majina mengine ya kizungu ni magumu kutamka hasa kwa ndimi zilizozoea kiswahili. Hata watangazaji wa BBC (English) nao huwa wanachemsha kutamka majina ya kiafrika: Kwa mfano 'Mkapa' utasikia wanasema 'Makapa' nk. Hata hivyo kama kioo cha jamii wanapaswa kujiandaa kabla.

The rest of your criticisms are true and fair.

Taib ..sheikh Taib..
 
alnadaby
mbona hukusema kuhusu kuonekana nchi nzima maana hii ni Tv ya serikali ! kuhusu kutamka majina nafikiri huo ni upungufu wa mtu binafsi na hata watangazaji wa tv maarufu duniani hupata shida kwa baadhi ya majina.
walipoanza walianza kwa kutangaza vipindi wakiwa wamevaa mavazi (waliyoyaita rasmi ya Kitaifa) sijui siku hizi yameenda wapi.
taarifa yenyewe ya habari mara ianze saa mbili kasoro mara ianze saa mbili na dakika tano. hawapo serious.
unaposema mpira mimi kama kuna mpira naangalia zangu kupitia TV ya mozambique maana pale mpira unaonekana vizuri kuliko TBC1. Ni mara ngapi umekaa kwenye runinga yako ukisubiri mechi waliyosema wataonyesha kumbe hawaonyeshi ? kwa mimi ni mara nyingi na hata last weekend walisema wangetangaza mechi ya real madrid baada ya mechi ya manchester na nikasubiri weee mwisho nikaamua kulala.
kwa mimi TBC1 no no no. naingalia tu kama mpira huo haupo katika TV zingine.
 
Kwa ujumla kuna improvement kwa TBC 1 ukilinganisha na ilivyokuwa.Kero zipo kwa Tv zote hapa nchini na ndiyo maana sikuegemea TBC 1 na nimekosoa na kushauri kwa upande wa Star TV pia.

Matamshi ni muhimu sana katika fani ya utangazaji.Kutamka jina au neno sahihi ni jambo zuri.
Kwa mfano kuna mtangazaji alitaja jina la Marat Safin kwenye kipindi cha michezo kwa kumuita jina la mwanzo lisivyotakiwa (Sikumbuki)kisha la pili akasema Safina.

Watazamaji huangalia Tv nyingi kwa hiyo wanayajua majina sahihi ya wengi ikiwa ni wanasiasa ,wanamichezo n.k.
 
Matamshi ni moja tu ya changamoto katika vituo vyetu vya runinga, lakini mengine zaidi ni ukamilifu wa habari zenyewe, aina ya habari wanazotupa - kwa sababu nyingine ni zile za kutangaza mambo ya wakubwa na hasa hasa kuwasifia, kutangaza maagizzo ya vigogo kwa walala hoi, lakini pia je habari zenyewe zinaandikwa katika hali ambayo mtazamaji anavutiwa kuendelea kuangalia?
 
Kwenye TV, kweli TBC wamejitahidi sana lakini mimi kwa upande wangu bado nakwazika na matangazo yao ya radio TBC taifa. Kumekuwa kunajitokeza mwangwi wakati fulani kwenye matangazo yao nina imani hili linahusiana sana mambo ya kiufundi.Ukisikiliza vipindi vya jioni kama michezo au taarifa za habari zao kunakuwa na mwangwi sana na matangazo kufifia...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom