TBC1 hawana pesa ya kurusha bunge ila wana pesa ya kumrusha Makonda

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Habari waungwana,
Niko hapa na weekend naperuzi channel zetu zina nini cha mimi kuweza kuangalia, wakati napitapita nikapita na TBC, chaneli yetu ya Taifa. Nakutana na Makonda anahutubia, akili ya mwanzo nikawaza labda Rais Magufuli yuko sehemu na Makonda kaalikwa.

Baadae inapita banner kuwa ni kikao cha Makonda na watendaji wa Halmashauri, dah kinarushwa live televisheni ya taifa. Nadhani tatizo lililopo TBC ni aidha kukosa priorities au kuleta siasa lakini si rasilimali fedha au kubana matumizi kama wanavyotuaminisha.
 
Hilo Halima shida kwani anataka aonekane kwamba anafanya kazi kwa bidii na ndiyo sababu amewapa order TBC wamtoe kwenye matangazo,na usijali kodi yako na yangu ndiyo iliyolipiwa.Halafu yule anayejiita Rais wa Malaika atampa pongezi.

Siasa za matangazo utendaji sifuri
 
Mlilalamika kusema kwamba rais kachagua wastaaf badala ya vijana kuwa wakuu wa mikoa lakin kati yao kuna mhe. Makonda ambaye ni kijana mwenzetu na lakn bado mnamponda na kusema hafai kabisa kuongoza mkoa kwa umri wake..tuelewe vipi sasa
 
Swali Ni Nani Amelipia Hiyo Live Coverage Ya Kikao Cha Makonda Na Wenyeviti Wa Mitaa, Vitongoji Na Vijiji Na Baadhi Ya Watendaji Wa Manispaa Za Dar!!! Maana Bunge Tumeambiwa Serikali Haina Pesa Za Kulipia Matangazo Yale!! Je, Haya Ya Makonda Ni Nani Analipia Gharama Zake!!!!!??
 
WAZIRI MWENYE DHAMANA NA TBC HAJUI MAANA YA" TFF" UNATEGEMEA NINI.
PENGINE NAPE HAKUMAANISHA KUWA TBC HAINA HELA MAANA HAJUI HATA NENO TBC NI NINI.TUNAMSUBIRI MISS TANZANIA!
MAKONDA MTOTO WA MAMA ZIWA HALITOKI MDOMONI.
AWAMU YA MASIFAAA!!!
 
Ukweli makonda ni bonge la hazna ya kiongozi wa baadae. Anaongea point sana sio kama akina kubenea
Elewa Hoja Kwanza, Alafu Uchangie Hoja!! Sio Kupayuka Tu Ktk Thread Za Watu!! Anzisha UZI Wako Wa Kumpa Sifa Bwanako!!!! Hoja Ya Mleta UZI Ni Gharama Za Kurusha Matangazo Hayo, Yanagharamiwa Na Nani!!!?? Makonda Mwenyewe, TBC 1, Ofisi Yake Au Wafadhali!!!!?? Sio Ubora Wake!!!!
 
Habari waungwana,
Niko hapa na weekend naperuzi channel zetu zina nini cha mimi kuweza kuangalia, wakati napitapita nikapita na TBC, chaneli yetu ya Taifa. Nakutana na Makonda anahutubia, akili ya mwanzo nikawaza labda Rais Magufuli yuko sehemu na Makonda kaalikwa.

Baadae inapita banner kuwa ni kikao cha Makonda na watendaji wa Halmashauri, dah kinarushwa live televisheni ya taifa. Nadhani tatizo lililopo TBC ni aidha kukosa priorities au kuleta siasa lakini si rasilimali fedha au kubana matumizi kama wanavyotuaminisha.
Habari waungwana,
Niko hapa na weekend naperuzi channel zetu zina nini cha mimi kuweza kuangalia, wakati napitapita nikapita na TBC, chaneli yetu ya Taifa. Nakutana na Makonda anahutubia, akili ya mwanzo nikawaza labda Rais Magufuli yuko sehemu na Makonda kaalikwa.

Baadae inapita banner kuwa ni kikao cha Makonda na watendaji wa Halmashauri, dah kinarushwa live televisheni ya taifa. Nadhani tatizo lililopo TBC ni aidha kukosa priorities au kuleta siasa lakini si rasilimali fedha au kubana matumizi kama wanavyotuaminisha.
Hicho kikao kitarushwa Massa mangapi na kwa siku ngapi tupige calculation za ulinganifu ili niku support
 
Hakuna haja ya kushangaa makonda kurusha live kikao maana anpenda sifa, kama aliweza kumchapa kibao Warioba kwenye kongamano lililokuwa LIVE kitu ambacho ni utovu wa nidhamu, itakuwa kuongea tu na kutoa maagizo ashindwe kurusha Live, jamaa atajionesha kwenye vyombo vya habari mpaka yeye ndio aonekane waziri wa habari, Nape kazi anayo ila wote wana fanana watajuana wenyewe.
 
Labda wanataka wengine wajifunze kwake.......si unajua Tanzania ilivyo na utajiri wa Watendaji Maroboti.
 
Back
Top Bottom