TBC1: Angalia Kamati ya Muafaka ya CCM

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
789
WanaJF; TBC1 wameahidi kurusha hewani kamati ya muafaka ya CCM walichoongea na waandishi wa habari kuhusu muafaka wa siasa kwenye visiwa vya Zanzibar...

Ni vyema wanaJF muyapate ninyi wenyewe moja kwa moja; kama mjuavyo vyombo vyetu vina-spin, hivyo ni vyema kuona, kwani ni tofauti na kusubiri mwenzako akutafisirie.

Wataonyesha baada ya Taarifa ya habari...ya leo Jumapili tarehe 11, Mei. 2008... huenda ikawa kuanzia saa tatu kasoro usiku saa za Dar es Salaam.
 
Endeleeni tu kunywa bia zenu popote pale mlipo ndugu zangu, there will be nothing new,surely you dont want to hear tha c..p again and s...w your fabulous weekend!
 
Endeleeni tu kunywa bia zenu popote pale mlipo ndugu zangu, there will be nothing new,surely you dont want to hear tha c..p again and s...w your fabulous weekend!

Mtu makini yeyote atapenda kusikia pande zote mbili! kukataa kusikiliza pande moja na kusikiliza moja ni unazi!!!
 
Mtu makini yeyote atapenda kusikia pande mbili!

Ni kweli kabisa unachosema, lakini CCM ni chama cha wababaishaji ambao siku zote wameweka mbele maslahi yao kama viongozi wa CCM ili watetee KULA na maslahi yao badala ya yale ya nchi. Kwa hiyo sidhani kama kutakuwa na jipya lolote.

Kamati ya CCM ya muafaka yailaumu CUF

Written by KLH News
Sunday, 11 May 2008
Kamati ya CCM iliyoshiriki katika mazungumzo ya muafaka wa Zanzibar imekilaumu chama cha CUF kwa kupotosha mwelekeo wa mazungumzo hayo. Akizungumzia juu ya suala Mwenyekiti mwenza wa mazungumzo hayo Mhe. Kingunge Ngombare Mwiru amekishangaa chama cha CUF kwa upotoshaji huo wa makusudi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Bw. Kingunge amesema kuwa chama cha CUF kimekuwa kikitoa matamshi kuhusu mazungumzo hayo kinyume na makubaliano ya kutoa matamshi kwa pamoja.

Pamoja na hayo, Bw. Kingunge amesema kuwa chama cha CUF kimezungumza na umma kana kwamba makubaliano yalikuwa yamekwisha fikiwa juu ya masuala muhimu. Mojawapo ya mambo ambayo Bw. Kingunge anadai yamepotoshwa na CUF ni lile la serikali ya mseto na nafasi ya Makamu wa Rais wa Zanzibar.

Pamoja na madai hayo ya Kingunge chama cha CUF bado kimeendelea kutoa msisitizo kuwa hakitarejea kwenye meza ya mazungumzo hadi pale ambapo Mwenyekiti wa CCM Mhe. Jakaya Kikwete atakapokuwa tayari kusimamia mazungumzo hayo yeye mwenyewe kwa kuwakutanisha mahasimu wa kisiasa wa visiwa hivyo kama alivyofanya katika suala la mgogoro wa Kenya pale aliposhiriki katika kuwaleta kwenye meza ya mazungumzo Bw. Mwai Kibaki na Bw. Raila Odinga

Mgogoro wa Zanzibar umedumu kwa muda mrefu hasa baada ya matukio yaliyotokea baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2000 na uchaguzi mkuu wa 2005.
 
Ni kweli kabisa unachosema, lakini CCM ni chama cha wababaishaji ambao siku zote wameweka mbele maslahi yao kama viongozi wa CCM ili watetee KULA yao badala ya yale ya nchi. Kwa hiyo sidhani kama kutakuwa na jipya lolote.

Nadhani mzee wangu utakuwa umekosa umakini wewe!!!! haya mzee wangu... kweli nchi inazama hata wale wanaokosoa nao ni watu wa kuangalia upande mmoja!!!!
 
Ambayo hayapo kwenye tovuti ya mwanakijiji ni pamoja na haya:

1. Wadau wa Muafaka ni (CUF, CCM, Rais wa Zanzibar, Rais wa Jamhuri na Mwisho Wananchi); sasa jiulizeni kama mwananchi angehusishwa je?

2. Kamati zilishakubaliana kwamba kamati hazikuwa na kauli ya Mwisho (Kauli za Mwisho zilikuwa zinatolewa na vyama,,, kupitia vikao vikuu vya vyama husika)

3. Makubaliano yoyote yalikuwa yatangazwe na makatibu wakuu wote wawili... (nothing go public unless there is a joint press conference with signed press)

4. Ajenga zilikuwa tano... nne tayari.

5. Agenda ya tano kukubalina Utaratibu wa utekeleza wa ajenga zote 1 hadi 4. Hivyo agenda ya tano ilikuwa haijaanzwa... so makubaliano yangekuwa wapi?

6. Kungekuwa na Makamu wa wiwili wa Rais, makamu wa Kwanza anatoka chama kilichochukua cha pili kwenye uchaguzi, na Makamu wa Pili wa Rais atatoka kwenye chama kitakachoongoza, yaani chama tawala... na makamu wa pili ndiye anaratibu wizara pamoja na kuwa mrithi wa Rais in case raisi akipatwa na jambo.

7. Kuwe na baraza la usuluhishe in case kama hakutakuwa na maelewano kati ya Rais na yule makamu wa kwanza wa Rais.

8. Kamati ya CCM ikapeleka maelezo ya hapo walipofikia... kama walivyokubaliana kwamba vyama ndio vyenye kauli za mwisho.

9. Halimashauri kuu inakubaliana na haya
i. Agenda zote nne zilivyozungumziwa. hivyo walikubali serikali shirikishi.
ii. Setup ya Serikali ... yaani ile inaondoa waziri kiongozi... na badala yake kuwe makamu wa Rais.

10. Marekebisho... Mapendekezo ya NEC.
a.. Marekebisho kwenye ile ya chama kushirikishwa kwenye baraza iwapo itapa kura...5% za rais... badala yake... Rais atumie vitu vya baraza la wawakilishi ya vyama vilivyopata... maana waweza pata 5% ya kura lakini usiwe na mwakilishi.
b. Kukiwa na baraza la wawasuluhishi kwa kuamua iwapo makamu wa rais wa kwanza na Rais watakuwa hawakubaliani... NEC wakasema... vyama ndio viwe wasuluhishi... nendeni mkazungumze na wenzenu (CUF) muelewane juu ya hilo.
c. Uratibu uliopo tulioridhi kutoka Uingereza ni ukishinda hata kwa kura moja unapata vyote,,, ukikosa kwa kura moja unakosa vyote... ndio utaratibu tulioridhi... Utaratibu huu maarufu unafanya kazi nchi nyingi... lakini ukweli haufanyi kazi Zanzibar... kwa sababu ya historia ya Utumwa, Matabaka, watwana, waungwana na kulikuwa na mgawanyiko mkubwa huko nyuma... hivyo kulizuka chuki na kutoaminiana tangu siku nyingi. Chaguzi zote za Zanzibar isipokuwa ya 1957 hizo zingine zote kila aliyeshindwa alikataa kushindwa... Kwa kuwa utaratibu wa Serikali shirikishi ni mfumo mpya kabisa wa Siasa Zanzibar. Basi pendekezeni namna ya kutekeleza hilo ili ifikapo uchaguzi unaofuata... utaratibu mpya utumike...

11. Haya ni maelezo tu ya ziada..
Matatizo yake ni:
- Historia,
- Kuwepo vyama viwili tu na vinavyokaribiana.
 
Nadhani mzee wangu utakuwa umekosa umakini wewe!!!! haya mzee wangu... kweli nchi inazama hata wale wanaokosoa nao ni watu wa kuangalia upande mmoja!!!!

Kama unaamini hivyo sawa, lakini ukweli kuhusiana na ubabaishaji wa CCM unajulikana. Pamoja na kuwa wengi wetu tungependa kuangalia pande zote mbili lakini tusisahau history ya CCM katika swala hili la muafaka. Ni miaka mingapi tangu mazungumzo haya ya muafaka yaanze? Kama kweli CCM wangekuwa na nia ya kufikia muafaka huu ni kipi kinacholeta mtafaruku wa kutofikia makubaliano?, inahijitaji miaka yote hii? :confused: CCM ni wahuni tu na mafisadi hawana jipya!
 
Mtu makini yeyote atapenda kusikia pande zote mbili! kukataa kusikiliza pande moja na kusikiliza moja ni unazi!!!

Afadhali nisiwe makini, ni kupoteza muda kuwasikiliza watu ambao unajua 99% of the time ni wasanii. Sitegemei jipya toka kwa watu kama akina Makamba.

Kama kufanya hivyo ni kukosa umakini, let be it.
 
kimsingi CUF na CCM hawawezi kutatua matatizo bila kufanyika vurugu kubwa Zanzibar na umwagikaji damu and this to me is prophetic.
 
Wanabodi,
Nimesoma mahojiano ya mzee Kingunge na hakika namuunga mkono kwa sababu CUF walifungiwa Kanya boya na wakalikubali wenyewe.
Hata siku moja (naomba kurekebishwa) sikumsikia kiongozi yeyote toka CCM akizungumzia uwezekano wa serikali ya Mseto ama kiti cha Makamu wa rais isipokuwa viongozi wa CUF.
Sasa yawezekana yule Mangula aliwaingiza mkenge wakauvaa na sisi wananchi ni lazima tuwe wakweli kwamba hatujawahi kusikia Kikwete wala viongozi wa juu CCM wakizungumzia serikali ya mseto isipokuwa nachokumbuka ni kutafuta suluhu ya kisiasa visiwani.
Nitarudia kusema kwamba CCM haiwezi kufikia muafaka kwa madai ya CUF kwa sababu wakikubali muafaka huo ni kukubali matokeo ya uchaguzi kuwa CCM walishindwa uchaguzi Zainzibar..
Na kama kuna ukweli ama haki yeyote ya jambo hili CUF walitakiwa kushikilia kamba baada ya uchaguzi kuhakikisha haki hii ya serikali ya mseto inatumika kama walivyofanya kina Rila Kenya ama Morgan Zimbabwe uchaguzi urudiwe. haiwezekani msubiri miaka miwili ndani ya utawala ndio mje na haki ambazo tayari imekwisha wathiri wananchi vya kutosha na sidhani kama Katiba yetu inaruhusu.
Hii inaonekana kama ni kutafuta ULAJI zaidi ya haki ile ya msingi wa kidemokrasia... Wakati wote huu wa miaka miwili yaani CUF walikuwa bado wakitegemea kuwepo kwa serikali ya mseto kweli bila kuvihusisha vyombo vingine vya kimataifa ama vyama vingine?.. Je hili lilikuwa deal kati ya CCM na CUF hali vyama vingine havifahamu sababu ya kufikia muafaka huo?..maanake kutokana na matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa CCM walishinda sasa huu muafaka wa mseto unatokana na matokeo yapi?...
 
Naomba kutofautiana na wewe. CCM plays propaganda.
Jee ni lini ulisikia CCM wakazungumzia lolote lile waliongelealo ndani ya close door? Kama CCM hawataki kuzungumzia swala la Balali au swala la kukabidhiwa kwao file liloonyesha fedha za EPA zimetumika kwenye uchaguzi wa 2005. CCM never told us anything. Ndivyo walivyo.

Mwanzo nilikuwa nakubaliana na swala la kupeleka kwa wananchi swala la muafaka. Lakini badaa ya kufanya smart analysis zangu nimeona hili swala ni political spin.

Imagine kwamba kwa miaka zaidi ya 15 pemba hawapati maji safi, umeme wa kutosha, mafuta, msaada wowote wa kijamii kutoka serikali kuu iliyopo unguja. Sababu serikali imejaa wawakilishi kutoka pemba.

Kingunge lost his bearings, i support CUF asilimia kutokurudi kwenye meza ya majadiliano. Kama Makamba na wenzie walikubaliana kwamba serikali ya mseto iundwe, then that is what suppose to be. Hakuna Kingunge wala ngombarimwilu.
 
kimsingi CUF na CCM hawawezi kutatua matatizo bila kufanyika vurugu kubwa Zanzibar na umwagikaji damu and this to me is prophetic.

Hakuna sababu ya vurugu CUF lazima wafanye kama Morgan Tsvangirai wa MDC kule Zimbabwe, kuwa makini na hakuna kura kuibiwa. Lazima watekeleze hilo kama wanataka ushindi huwezi kila siku kulia Nyau wakati unaachia mianya ya wizi wa kura. Kuna utawala wa kimabavu kama wa Mugabe? Wajipanga wawang'oe madarakani - mbona Pemba wameweza?
 
Nami naamini kama wewe kwamba muafaka unaweza kufikiwa bila vurugu, tatizo kubwa nilionalo ni CCM kulivuta hili jambo kwa mwendo wa konokono ili lisiamuliwe mpaka uchaguzi wa 2010. JK ndiyo kiongozi wa juu CCM kama angeona umuhimu wa muafaka basi angechukua usukani mwenyewe na kuwaweka pembeni Makamba na Kingunge ambao hawana uwezo wowote zaidi ya kulinda maslahi yao kama viongozi na yale ya chama chao. Kama alivyosema Jaji Warioba ukiwa kiongozi ni lazima wakati mwingine ufanye maamuzi mazito bila kuogopa kulaumiwa na wafuasi wako. Cha muhimu ni kwamba maamuzi hayo yafanywe kwa kuweka mbele maslahi ya nchi badala ya kitu kingine chochote kile.
 
kimsingi CUF na CCM hawawezi kutatua matatizo bila kufanyika vurugu kubwa Zanzibar na umwagikaji damu and this to me is prophetic.

Heshima mbele Mzee Mwanakijiji,nadhani utakuwa na muono mfupi kama utafikili hatuwezi kutatua matatizo yetu wenyewe kidemoklasia mpaka tumwage damu.
kumbuka tumeshawahi kutatua matatizo mengi zaidi kabla ya hili hivyo nadhani usuruhishi utapatikana is just a matter of time, tunawatu walio onyesha uwezo wa kufanya hivyo
 
Mchelea Mwana,

Mzee Mwanakijiji amepoteza dira na matumaini, anatuombea tulioko mwanakwerekwe twende kule buguruni kwenye kipindupindu kila mvua zikinyesha!!!

Mzee tunaweza tatua matatizo yetu bwana... waambie CUF na CCM waendelea kumalizia Agenda ya Tano.
 
Back
Top Bottom