Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,565
Wanabodi,
Heri ya Pasaka,
Mara moja moja huwa ninatembelea Kituo cha TBC kwa shughuli zangu, leo Jumapili ya Pasaka nimepita pale na kuushuhudia bonge la OB Van mpya ya Kufa Mtu ikitua TBC!, kwa maelezo ya juu juu, OB Van hii, ina Kamera 12!, na moja ya camera hizo ni camera ya slow motion. Itarusha HDV Signal Kama DSTV.
Gari hili na vifaa vilivyomo ndani yake, vitaifanya TBC kuwa ndicho kituo cha Televisheni cha kwanza nchini Tanzania, kinachoongoza kwa vifaa bora vya kisasa vinavyotumia teknolojia ya kisasa hali ya juu ya full HD.
Kituo kingine chenye vifaa vya full HD ni Azam TV ila wao OB Van yao ni ya kamera 8!, hivyo hivyo hii OB Van ya TBC ya kamera 12, ndio OB Van funga kazi kwa Tanzania kwa sasa!.
Japo uongozi wote wa juu wa TBC ulikuwepo kushuhudia OB Van hiyo ikishuka, mimi sikuweza kuuliza lolote kuhusu OB Van hii zaidi ya kuikodolea tuu macho, maana sicho kilichonipeleka mahali hapo siku hiyo!.
Haya ndio baadhi ya mambo yake!.
Kwa gari hili, sasa TBC ndio inapaswa Televisheni kiongozi kwa Tanzania kwa kuwa the best TV Station in Tanzania kwa sababu ndio yenye vifaa bora na the best kuliko TV nyingine yoyote nchini Tanzania!, ila kiukweli, kuwa na vifaa bora ni jambo moja, kuwa na watu wenye uwezo wa kuvitumia (technical) hivyo vifaa bora ipasanyo ni jambo jingine!, yaani TBC kuwa na maproducer creative na ma talented presenters wa kutosha wenye uwezo, ari, moyo, na vipaji vya kuvishibisha vifaa hivi pia ni jambo jingine!.
Mabingwa wa utangazaji duniani, the BBC, waliishaligundua hili siku nyingi, hata uwe na vifaa vya kujaa kutoka duniani hadi mbinguni, pekee yako hauwezi!. Wanachofanya BBC, ili kupata the best kutoka kwenye market, wana commissions outside producers na presenters wazuri, kuwaletea a diverse contents kwa sababu wao peke yao, hawawezi!. Vivyo hivyo, TBC lazima uendelee kufungua milango yake kwa outside producers/presenters wenye creativity na vipaji vya hali ya juu kuleta a diverse contents.
TBC wao wenyewe tuu wao kama wao, hawawezi, ndio maana mnawaona kina Joti, wamehama kutoka EATV sasa wako TBC, na wakati wa maonyesho ya Saba Saba na Nane Nane, mnawaona watu kama Pasco Mayalla na PPR akivurumisha vipindi TBC, hivyo TBC iendelee kufungua milango yake na sisi Tanzania tuwe na Soap Opera zetu kama Isidingo kwa kila mwenye uwezo, kipaji alete vipindi TBC na wengine wengi upcomming talents wafuatie.
Paskali.