TBC wizara kuhamishwa kwenye nyumba si habari muhimu?.

HGYTXK

Senior Member
Oct 3, 2011
194
70
ITV wametuonyesha jinsi wizara nyeti ya serikali yetu ikifukuzwa na kutolewa nje ya ofisi walizopanga toka kwa NHC kwa kushindwa kulipa pango la mil 30,cha kushangaza television yetu ya taifa inayoendeshwa kwa kodi zetu haikuona habari hii kuwa ni ya umuhimu kwa taifa.ACHENI KUFICHA UOZO NYIE.
 
Wizara ya Kilimo(Elimu Kwa wakulima) imefukuzwa kwa kudaiwa mil 30 za pango,aibu bil3 wametumia igunga
 
Ni zaidi ya Ze comedy,hii serikali yetu bwana!,TBC nayo ni ZERO kabisa.
 
Wanazionea sana taasisi za serikali miaka yote ukute hapo hata umeme maji hawalipi kabisa kama wizara zinavyofanya bajeti za hizo vitu wanazipeleka puani!!
 
Umekariri kuwa habari ikionekana ITV ni lazma pia ionekane TBC!!
 
Nape jae atuambie hizo Bil 3 wamezitowapi kama sio kuiba kodi zetu. Hii nchi mwisho wake tutakuja kutoa macho na kuvunjana mikono kama tusipo Watoa hawa Mafisadi kinguvu. Mungu Ibariki Nchi yangu ya Tanganyika tupo kwenye wakati mgumu sasa.
 
Wale jamaa wanaitwa "UKULIMA WA KISASA" yaani Serikali inayotumia ma Bilioni kwenye kampeni inashindwa kulipia 30 Milioni tu??? Nasikia hao jamaa ndioo wanaotengeneza vijarida, kalenda na vipeperushi vyote vya masuala ya Kilimo lakini hawana fungu la kulipia pango..ni fedheha kubwa sana!!..TBC wasingeonyesha hilo ni aibu ya Taifa, NHC ni ya Taifa na hao WIZARA YA KILIMO ni SERIKALI...TBC ndo haswaaa kwa kulinda aibu ya Serika;li yao wapo mbele. Hpo mfuatilie mtasikia tu mtu lazima atang'olewa ofisini kwa Uzembe wa makusudi hata kama bajeti haikuwepo watamwambia "kwa nini hukuleta taarifa unadaiwa fedha kidogo hizo mpaka tuna hadhirika??" Magamba kwa unafiki si mnawajua??.
 
Umekariri kuwa habari ikionekana ITV ni lazma pia ionekane TBC!!

Acha uvivu wa kufikiri ww,ni chombo kipi kinapaswa kutoa habari za umma kwa kipaombele kama sio chombo cha umma?,wapo watu kama ww mikoani huko hawatazami station yeyote zaidi ya Tbc watapata wapi habari za serikali yao?.Acha unazi wa kuburuzwa kaka.
 
Ubarikiwe sana Mchechu. NHC inaongozwa na vijana ndo maana tunaona maendeleo. Si Wasira alikuwa humu? Je, Mwapachu?
 
hahahah KILIMO KWANZA matokeo yake ni Igunga kwanza kwa bilion 3 alafu kilimo baadae tutalipa mil 30 ya pango.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom