TBC: Wamasai na Wahadzabe ni kivutio cha Watalii?

Njemba Soro.

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
3,246
5,756
Hivi kweli televisheni ya Taifa mnashindwa kwenda hata Mabwepande kupiga picha wale nyoka, hata hapo Saadani kupiga picha wale Tembo?

Eti mnasema Wamasai na Wahadzabe ndio kivutio kweli? Hivi hamuoni aibu? Kwani nyie TBC Safari Chaneli mnatumia flash? Mbona hamna jipya nyie?

Huu uzembe mnaufanya kwa kuwa mnakula kodi ya Serikali? TBC jichunguzeni, mjitambue kabla hamjatumbuliwa. Hamna jipya TBC.
 
Ungekua unajua Maana ya utalii usinge uliza swali la kipuuzi na kutoa Suggestions za kipuuzi namna hii.

Katika Aina za utalii kuna utalii wa Utamaduni. Sasa utamaduni unadhani ni wa Wanyama??

Refer forms of Tourism. Utaelewa kuna utalii wa aina ngapi.

Utalii hauishii kuja kuangalia Wanyama na milima.

Kuna utalii wa matibabu, utalii wa Michezo, wa ngono, utalii wa kimasomo, utalii wa Wanyama, utalii wa Fukwe, utalii wa Natural Features and all many.

So usijifunge kwenye kabati la utalii wa wanyama
 
Hiyo ni legacy ya Nyerere, hakuna mtu alituchukia na kutudharau Waafrika kama Nyerere, Nyerere kama Mandela wote ni saleouts!
 
Ungekua unajua Maana ya utalii usinge uliza swali la kipuuzi na kutoa Suggestions za kipuuzi namna hii.
Katika Aina za utalii kuna utalii wa Utamaduni. Sasa utamaduni unadhani ni wa Wanyama??
Refer forms of Tourism. Utaelewa kuna utalii wa aina ngapi.
Utalii hauishii kuja kuangalia Wanyama na milima.
Kuna utalii wa matibabu, utalii wa Michezo, wa ngono, utalii wa kimasomo, utalii wa Wanyama, utalii wa Fukwe, utalii wa Natural Features and all many.
So usijifunge kwenye kabati la utalii wa wanyama
Naongezea na siasa pia,kama alivyoainisha kp huko UN na chama chetu kinavutia watalii
 
Hivi kweli televisheni ya Taifa mnashindwa kwenda hata Mabwepande kupiga picha wale nyoka, hata hapo Saadani kupiga picha wale Tembo?

Eti mnasema Wamasai na Wahadzabe ndio kivutio kweli? Hivi hamuoni aibu? Kwani nyie TBC Safari Chaneli mnatumia flash? Mbona hamna jipya nyie?

Huu uzembe mnaufanya kwa kuwa mnakula kodi ya Serikali? TBC jichunguzeni, mjitambue kabla hamjatumbuliwa. Hamna jipya TBC.

Ni kweli huu ni ujinga mtupu.
 
Akili yako ikisikia utalii anakimbia kwenye wanyama?

Wamasai ni jamii ya watu waishio kwenye hifadhi pamoja na wanyama hii tu inatosha kushangaza mtu, Wamasai ni jamii ya watu ambao utamaduni wao umeegemea zaidi kwenye kudumisha mila zao na ni rahisi kuwatambua kwa maisha yao.

Utalii ni neno pana zaidi ya ujuavyo, umewahi kusikia utalii wa fukwe? Hizo jamii mbili ulizotaja nadhani huzijui vizuri.
 
To be honest Chanel ya safari imepiga hatua kubwa ukilinganisha na ilivyoanza ila bado safari ni ndefu. Napendekeza kuwe na subtitles za kiingereza, pia vipindi viongezwe na viboreshwe.
 
Wamasai kufanywa kivutio kwa watalii, ni sawa na miaka ya nyuma yule mtoto mweusi kufanywa kivutio kwenye museum kule USA. Akifananishwa na kima, Huwezi kumfanya binaadamu mwenzio kama kivutio. Na sisi tuombeni visa ya kwenda USA kuwaona wa Amish kama kivutio pia basi.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Kweli Utamaduni ni utalii. Ila kuna kaukakasi fulani huwa napata pale binadamu anapotumika moja kwa moja kama kivutio cha utalii. Yapasa tuende kwa upana wa utamaduni na sio watu. Wakati binadamu wengine wakisonga mbele kimaendeleo kuwachukua wenzetu kama mateka kwa mgongo wa utalii inanipa ukakasi. Ni hadi lini tunadhani tutaendelea kuwaona wenzetu wakiishi maisha ya porini kwa kisingizio cha kudumisha mila? Ni hadi lini tutaendelea kuona wakiishi katika makazi duni na huduma za afya duni kwa kisingizio cha utalii? Huo utalii utamaduni wauwezi hifadhika kwa njia zenye kuwapa staha ndugu zetu tukiwapa fursa za kimaendeleo? Leo tunazungumzia bima ya afya kwa wote hapo hapo tunataka wenzetu waendelee kuishi kama zamani, eti tunadumisha mila!!! Kuenzi utamaduni sawa, ila hebu tuache kuchukulia ubinadamu wao kama utalii, tujitambue, huyo anayekuhamasisha utalii wa utamaduni wa kuja kumuona binadamu mwenzake kama kivutio ujue kaweka dharau nyuma ya dhana yake!! Ni mtazamo wangu
 
To be honest Chanel ya safari imepiga hatua kubwa ukilinganisha na ilivyoanza ila bado safari ni ndefu. Napendekeza kuwe na subtitles za kiingereza, pia vipindi viongezwe na viboreshwe.
Hilo ni kweli kabisa. Ubora wa picha ni wa kiwango kizuri japo siyo sana ila huwezi kulinganisha na TBC1.

Wakiendelea na moto huo watafikia mbali.
 
Ungekua unajua Maana ya utalii usinge uliza swali la kipuuzi na kutoa Suggestions za kipuuzi namna hii.

Katika Aina za utalii kuna utalii wa Utamaduni. Sasa utamaduni unadhani ni wa Wanyama??

Refer forms of Tourism. Utaelewa kuna utalii wa aina ngapi.

Utalii hauishii kuja kuangalia Wanyama na milima.

Kuna utalii wa matibabu, utalii wa Michezo, wa ngono, utalii wa kimasomo, utalii wa Wanyama, utalii wa Fukwe, utalii wa Natural Features and all many.

So usijifunge kwenye kabati la utalii wa wanyama
labda kama kweli hakuna cha kutangaza ili kuvutia ........ unamaanisha hadi ngono ni utalii?? Hivi we jamaa hujui kwamba kuna watanzania hawajui hata faida za utalii.... KWELI UNAWEKA WAMASAI W
Akili yako ikisikia utalii anakimbia kwenye wanyama?

Wamasai ni jamii ya watu waishio kwenye hifadhi pamoja na wanyama hii tu inatosha kushangaza mtu, Wamasai ni jamii ya watu ambao utamaduni wao umeegemea zaidi kwenye kudumisha mila zao na ni rahisi kuwatambua kwa maisha yao.

Utalii ni neno pana zaidi ya ujuavyo, umewahi kusikia utalii wa fukwe? Hizo jamii mbili ulizotaja nadhani huzijui vizuri.
bado utadai wazungu ni wabaguzi..... HALAFU HILI NI TATIZO KUBWA KUMBE?? Wamasai wanaishi na wanyama kwani wao ni wanyama??? JISHTUKIE BASI AISEE.
 
Hivi kweli televisheni ya Taifa mnashindwa kwenda hata Mabwepande kupiga picha wale nyoka, hata hapo Saadani kupiga picha wale Tembo?

Eti mnasema Wamasai na Wahadzabe ndio kivutio kweli? Hivi hamuoni aibu? Kwani nyie TBC Safari Chaneli mnatumia flash? Mbona hamna jipya nyie?

Huu uzembe mnaufanya kwa kuwa mnakula kodi ya Serikali? TBC jichunguzeni, mjitambue kabla hamjatumbuliwa. Hamna jipya TBC.
Yaani hawa jamaa wanakula tu kodi yetu bure, hii channel hata sijui kazi yake nini, kila ukiwasha tv unakutana na vipindi vilevile kama sio gombe kigoma basi kitulo iringa, haina mvuto kabisa.
 
Back
Top Bottom