TBC wakata matangazo wakati Meya wa Jiji akiongea

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Leo nimeshangaa,wakati wa uzinduzi wa daraja la Kigamboni, wakati Mayor wa jiji amekaribishwa kutoa salamu TBC waka freeze halafu wakaweka matangazo ya biashara na alipokuja DC wakaendelea,..

Mimi ni mwana CCM ila mlichokifanya mnatuumiza sisi wana ccm kukitetea chama kwa hoja ila vioja..kama hamuoni aibu sisi tunaona, mnatupa wakati mgumu sana mitaani
 
Nafuatilia ufunguzi wa daraja la kigamboni, Makonda kaanza kutambulisha wenyeji kwa rais, lakini la ajabu katika karatasi alonayo Makonda kwa vyovyote vile haikuwa na jina la Meya wa jiji.

Hata hivyo Makonda akamuona Meya wa jiji, kwa hivyo akamuita asalimie, ile kuanza kusalimia tu, AZAM na TBC matangazo yakakata, hayakurudi hadi pale Meya wa jiji alipo maliza.

Shaka yangu, huenda hii ni hujuma kwa Meya wetu wa jiji.... nawaza tu........
 
Aibu sana sana kwa taifa hili kwa kweli imetia kinyaa sana sikutegemea wanaweza kuufanya unyama huu i hope halitajirudia...mambo madogo madogo haya hufanya.serikali ichukiwe na uzalendo kupotea
 
Hata Makondo katika utambulisho wake ameonyesha wazi kumbagua Meya wa jiji.
Nadhani sasa ni wakati wa tit for tat, hakuna cha kujikomba wala kujifanya waungwana kwa watu wasio waungwana.
Dar inafahamika kuwa upinzani ndio wenye nguvu na mamlaka jee wangejisikiaje kama Mwenyekiti wa ccm anatambulishwa kisha anazomewa mbele ya wageni? Huo ni mradi wa serikali, hata kama TLP ingeingia madarakani lazima ingemaliza ujenzi. Ni ujinga kuleta uchama katika mambo ya kitaifa.
Hivi mbona ccm inataka kuleta matengano miongoni mwa jamii?
Waelewe kuwa ni bahati mbaya kuwa upinzani ndio unawanachama wengi vijana na hao ndio wanauweza UHUNI jee wataweza kuhimili?
 
Back
Top Bottom