Elections 2010 TBC waandaa wananchi kukubali matokeo, wawachafua CHADEMA!

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,529
8,614
Leo TBC Wameanza rasmi vipindi mfululuzo vya kuwaandaa wananchi kuyakubali matokeo....kwa mtu aliyesomea mawasiliano atagundua pia kuwa kampeni yao inahusisha kuonesha image mbovu kwa vyama vya upinzani hususani CHADEMA ,...ila inaonekana wanaonekana kuiinua CUF JUU!!

Kipindi cha VIMBWANGA VYA UCHAGUZI kimeanza kikiendeshwa na waandishi akiwemo MARINE HASSAN ...wameonesha vyama viwili tu namna mikutano yao ilivyokuwa CUF na CCM.

Kinafuatia kipindi cha suzy mongy kinaitwa HAIKUWA RAHISI....nacho malengo na maudhui ni hayo hayo.....na vipindi na makala hizi zitaendelea hadi jumamosi....

Ni wazi kuwa huu ni mpango mahsusi wa kuwavunja moyo watu wa bara ...kuwa chama wanachokiunga mkono ..si lolote.....

Tunayo safari ndefu...!!
 
TBC vipindi mfululizo
1. Vimbwanga vya CCM na NEC Kuchakachua katika uchaguzi 2010
2. Haikuwa Rahisi CCM na NEC Kuchakachua katika uchaguzi 2010
 
TBc huwa siangalii, kwa sababu nathamini afya yangu, ... sina haja ya kujipa ghadhabu bila sababu za msingi.
 
Mimi nna mwezi wa tatu sasa siangalii TBC, najua PAYE yangu kwenye Mshahara inawalipa hawa akina Marine hassan. Ipo siku itawatokea puani huu mtindo wao wa ushabiki wa vyama
 
Unajua kiukweli katika uchaguzi huu ameshindwa ccm,wakaiba kura kutimiza uchu wao wa madaraka na kuwaibia watanzaini,sasa wameanza uongo.Tatizo lao ni wajinga sana hawajui kutathmini mambo,hawaoni mbali ndio maana wanahaingaika na mambo madogo madogo wana hofu kwa dhambi waliyoifanya lazima watunge uongo kwa watanzania lakini hawataeleweka Tanzania hii inajua maovu yao mengi na mbinu chafu.Waseme wanavyotaka kuhusu chadema ila serekali hii inayoingia kwa wizi itajuta,walikuwa wabunge wanne sasa zaidi ya 20.Nguvu inaanzia bungeni,kwenye kutunga sheria,kumpa raisi mamlaka au kumwondolea,sasas wala la tume huru litakapokuwa limewekwa sawa ndio watazinduka usingizini.Walimwita doc Slaa mwehu,mzushi angalia leo keshawaumbua saana.kabaki huyo anayejifanya kupendwa na watanzania wote kila mahali kashinda yeye tu,akawadanganye wajinga wenzie kina makamba na rz1.wizi mtupu!
 
Sio kazi rahisi sana kugeuza fikra za wau juu ya mambo yanayoendelea kwa kutumia vipindi tu. Watu wanataka kuona mabadiliko ya dhati kabisa kwa vitendo.
 
wanapoteza muda wao kwa watanzania ninavyowajua hawana muda wa kuangalia siasa kwenye vz wao ni tamthilia na mziki tu
 
Ni kweli na ni dhahili kwamba chama cha democrasia na maendeleo "chadema" ndicho kinachoongoza ktk uchaguzi huu wa tanzania bara,na ndio maana nec wamesuasua mno kutangaza matokeo na lengo lao kubwa ni kuchakachua matokeo.,..,...,
 
TBC-
T= tetea ufisadi
B=babaisha umma kwa uongo
C= Chakachua habari na matokeo ya kura
TBC na BBC ni mapacha walioshikana, kazi yetu kubwa sis madaktari ni kuwatenganisha ili kila mmoja aishi maisha yake. Operation hii ni kubwa itachukua masaa zaidi ya 6. matokeo ni kupona au kupoteza maisha.
Mbegu ya chuki inajengwa na TBC kwa kuunga mkono upotoshaji wa matokeo. Unamwona Marine akisisitiza sana kila anapotangaza DK feki kashinda. tena anachekelea saaaana na kujifanya nguli wa watangazaji. Saa ya ukombozi imefika amkeni msisikilize propaganda kudumaza mawazo ili tusahau kuwa tumeibiwa kura zetu. Dr.Slaa wa ukweli tuko na wewe usivunjike moyo.
 
Mimi siangalii tbc one ingawa nina king'amuzi chao.
ila akina marine ni makada wa ccm damu.
waacheni tu maana si wanakaa mtaani????!!!! watajijua huko na watu wa mtaani kwao.
 
Na wao watakuwa kama Habari Leo, uhuru, Mzalendo na Daily news tu

Mh. KING KINGO, hao TB (ugonjwa), aaah! sijui TBC vile wanajiita, SIO WATAKUWA KAMA,....BALI WALISHAKUWA KWENYE KAPU MOJA LA HIVYO VIJIGAZETI FISADI. HATA hivyo WATANZANIA HALISI, hawana muda nao, wataendelea kuwapuuza hao watumwa wa fikra na waganga njaa.
 
TBC-
T= tetea ufisadi
B=babaisha umma kwa uongo
C= Chakachua habari na matokeo ya kura
TBC na BBC ni mapacha walioshikana, kazi yetu kubwa sis madaktari ni kuwatenganisha ili kila mmoja aishi maisha yake. Operation hii ni kubwa itachukua masaa zaidi ya 6. matokeo ni kupona au kupoteza maisha.
Mbegu ya chuki inajengwa na TBC kwa kuunga mkono upotoshaji wa matokeo. Unamwona Marine akisisitiza sana kila anapotangaza DK feki kashinda. tena anachekelea saaaana na kujifanya nguli wa watangazaji. Saa ya ukombozi imefika amkeni msisikilize propaganda kudumaza mawazo ili tusahau kuwa tumeibiwa kura zetu. Dr.Slaa wa ukweli tuko na wewe usivunjike moyo.
Kilichokuja Tanzania siyo BBC bali ni CCM tawi la London ambao wameajiriwa na BBC. Ni maswahiba wa bosi wao wa zamani Tido Mhando ambaye sasa ndiye mkurugenzi mkuu wa propaganda wa CCM kupitia TBC. Hili ni ushahid kuwa pweza lenye mikono mingi la CCM limejichimbia kila mahali na kazi ya kujinasua nalo ni kubwa lakini itawezekana tu. Kuna mambo makubwa matatu ya kuyafanya katika kipindi cha miaka mitano ijayo: (1) Kutafuta Katiba Mpya bila kukubali ichakachuliwe na CCM (2) Tume huru ya uchaguzi yenye uwakilishi wa vyama vyote vikuu na asasi zingine (3) Mikakati thabiti ya kutwaa majimbo mengine kutoka mateka ya CCM. Lazima uchaguzi wa 2015 ufanyike katika mazingira ya uhuru zaidi. Na kwa hili hatuhitaji msaada wa wafadhili/wahisani/wadau wa maendeleo, whatever!!!! Mapando yetu sisi wenyewe bila woga au kudanganywa na propagnda za CCM yataleta mafanikio. Tuache woga.
 
Ombi langu kwa wanaCHADEMA na wapenzi wa mageuzi wote popote walipo. Tafadhali anzisheni vyombo vya habari hasa vya kielektroniki, yaani Radio na Television, ili kupambana na propaganda za hewani zinazofanywa na vyombo vya habari vya CCM, serikali yake pamoja na vile vya mafisadi washirika wao. Uchaguzi huu umetuonyesha umuhimu wa kuwa na vyombo ambavyo havitatishwa na dola adharani au kwa kificho. Gazeti la Mwanahalisi limekwishaonyesha njiia. Ninawaomba na vijana wenye utaalamu na uwezo waanzishe websites (pamoja na majukwaa ya kijamii jama JF) zitakazosambaza habari za mapambano kwa urahisi. Nina uhakika uwezo huo upo.
 
Akiwepo Marine Hassan tutarajie nini! binafsi niliacha kuangalia TBC hasa kipindi hiki cha uchaguzi maana unaweza pasua TV
 
The can only fool us once, BUT they can't fool us Forever!!

TBC hawana weledi wowote kwenye tasnia ya habari na hao watangazaji wanalinda tu ugali wao ila wanamjua vema Dr. Slaa na chadema na miaka hii mitano ujayo watakosa cha kureport kutokana kwamba chadema imeweka makombora ya kutosha bungeni na imekamata majimbo muhimu Tanzania, zanzibar pia huu ni mwanzo wa mwisho wa ccm cuf wapo mchezoni sasa hakuna upenyo wa kuiba kura tena chaguzi zijazo.
 
Tunawajua vizuri hao TBC, sio TBC ambao wamekua wakizima mijadala mbali mbali ya LIVE kutoka bungeni hasa akiwa anachangia mbunge wa upinzani(i.e Zitto)? sio TBC ambayo imeendesha mahojiano na mafisadi ya kuwasafisha na kuyaita exclusive? sio hao hao TBC wameshindwa kuonyesha hali halisi ya mtanzania huko vijijini na kubaki kuonyesha viprogram vyao vya padep na mkukuta kwenye kata zisizo zidi tatu?
:nono:
 
Leo TBC Wameanza rasmi vipindi mfululuzo vya kuwaandaa wananchi kuyakubali matokeo....kwa mtu aliyesomea mawasiliano atagundua pia kuwa kampeni yao inahusisha kuonesha image mbovu kwa vyama vya upinzani hususani CHADEMA ,...ila inaonekana wanaonekana kuiinua CUF JUU!!

Kipindi cha VIMBWANGA VYA UCHAGUZI kimeanza kikiendeshwa na waandishi akiwemo MARINE HASSAN ...wameonesha vyama viwili tu namna mikutano yao ilivyokuwa CUF na CCM.

Kinafuatia kipindi cha suzy mongy kinaitwa HAIKUWA RAHISI....nacho malengo na maudhui ni hayo hayo.....na vipindi na makala hizi zitaendelea hadi jumamosi....

Ni wazi kuwa huu ni mpango mahsusi wa kuwavunja moyo watu wa bara ...kuwa chama wanachokiunga mkono ..si lolote.....

Tunayo safari ndefu...!!

Mbona magazeti ya Mwananchi, Nipashe, MwanaHalisi na television ya ITV ilipokuwa inailia kobisi CUF mlikuwa hampigi kelele?

Acheni kelele zenu na badala yake :tape: midomo yenu! Hamna jipya isipokuwa maneno ya wakosaji tu!
 
Back
Top Bottom