Kalunguine
JF-Expert Member
- Jul 27, 2010
- 2,543
- 134
Siku ya ijumaa wiki iliyopita tarehe 2/9/2011, katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku, TBC radio walimpigia kampeni mgombea wa ubunge jimbo la Igunga kupitia CCM. Katika kumpigia kampeni, TBC radio walitumia taarifa ya habari yao wakimruhusu Malecela aliyeitisha mkutano wa waandishi wa habari huko Dodoma kupiga kampeni za mgombea huyo wa CCM. Katika taarifa hiyo, pamoja na mambo mengine, Malecela aliwahimiza wananchi wa Igunga kumchagua Dr. Kafumu ili CCM iweze kulikomboa jimbo la Igunga.
Sina hakika kama tarehe hiyo (2.9.2011) NEC ilishatangaza kuanza kwa kampeni hadi radio ya taifa ianze kumpigia kampeni mgombea wa CCM. Kama muda wa kampeni ulikuwa bado tendo hilo la TBC halikuwa ni ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi? Hivi Chadema wana habari na kampeni hii iliyofanywa na radio ya TBC kabla ya NEC kutangaza kuanza kwa kampeni?