TBC radio yampigia kampeni mgombea wa CCM jimbo la Igunga kabla ya tangazo la NEC

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
Siku ya ijumaa wiki iliyopita tarehe 2/9/2011, katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku, TBC radio walimpigia kampeni mgombea wa ubunge jimbo la Igunga kupitia CCM. Katika kumpigia kampeni, TBC radio walitumia taarifa ya habari yao wakimruhusu Malecela aliyeitisha mkutano wa waandishi wa habari huko Dodoma kupiga kampeni za mgombea huyo wa CCM. Katika taarifa hiyo, pamoja na mambo mengine, Malecela aliwahimiza wananchi wa Igunga kumchagua Dr. Kafumu ili CCM iweze kulikomboa jimbo la Igunga.


Sina hakika kama tarehe hiyo (2.9.2011) NEC ilishatangaza kuanza kwa kampeni hadi radio ya taifa ianze kumpigia kampeni mgombea wa CCM. Kama muda wa kampeni ulikuwa bado tendo hilo la TBC halikuwa ni ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi? Hivi Chadema wana habari na kampeni hii iliyofanywa na radio ya TBC kabla ya NEC kutangaza kuanza kwa kampeni?
 
Toka aondoke mstaarabu MHANDO amendoka na ustaraabu wake kilichobaki sasa ni TBC isiyo na maadili ya utangazaji hata mimi sasa sipotezi mda kuitazama kwa vile imejaa kushabikia MAGAMBA,TBC IMEKOSA DIRA BAADA YA KUONDOKA MHANDO
 
kwa ushahidi huu, chama makini kama cdm wamepaswa ku-compile huo ushahidi na kuufikisha ngazi husika ili process za disqualification zifanywe haraka bila kuchelewa.
 
Ni makosa kuanza kampeni ya aina yeyote ile kabla ya siku ikithibitika ni kweli mgombea wa CCM anaweza kuwa disqualified.
 
TBC= Tanzania Bila Ccm Inawezekana. Tirdo mhando aliisimamia hiyo akawa mwiba kwa magamba wakamtimua bila hata kuzingatia mkataba wake, igunga hawadanganyiki.!
 
Hata wapige kampeni kutokea angani!!! Hamna kitu wataona labda wachakachue kama kawaida yao!!!
 
media zote pro magamba wameshaanza kitambo hata michuzi, clouds and udaku shigongo
 
media zote pro magamba wameshaanza kitambo hata michuzi, clouds and udaku shigongo
 
media zote pro magamba wameshaanza kitambo hata michuzi, clouds and udaku shigongo

TBC ni chombo cha walipa kodi wote haipaswi kuvunja sheria ya uchaguzi na hasa kupiga kampeni kabla ya muda wake.
 
Sioni tatizo kwasababu mbona hata BBC walimpitisha David Cameron wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu Uingereza? Ikumbukwe kuwa TBC ni chombo cha serikali inayoongozwa na CCM, sasa kama a=b na b= c then automatically a=c.
 
Sioni tatizo kwasababu mbona hata BBC walimpitisha David Cameron wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu Uingereza? Ikumbukwe kuwa TBC ni chombo cha serikali inayoongozwa na CCM, sasa kama a=b na b= c then automatically a=c.

Ona we mwehu: True + False = False
False + True =True, Lakini True + True = False, na mwisho; False - False = True, uwe na akili kaka...
 
Unataka wawe timu ya CDM?.Mbona Tanzania daima wanapiga kampeni kila siku tena hata kabla ya kampeni kuanza
 
Back
Top Bottom