TBC ni Chombo cha Habari cha kupuuzwa mno

Mngurimi

JF-Expert Member
May 27, 2020
819
789
Habari wakuu,

Leo tarehe 28 Agosti, ilikuwa ni siku rasmi ya ufunguzi wa kampeni za uchaguzi kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika jiji la Dar es Salaam. Kampeni zimeanza jioni katika uwanja wa Zakhiem-Mbagala.

Kwa sisi tulio mbali na jiji la Dar es Salaam, kiu kubwa ilikuwa ni kupata matangazo ya moja kwa moja yakionesha tukio zima la ufunguzi wa kampeni hizo ili kusikiliza sera za wagombea na kuwapima kimaono. Katika pitia pitia channel kadhaa za hapa nchini, kwa bahati nzuri nikaweka TBC1 na nimefurahi sana kuona wakirusha live tukio lile.

Kitu kilichoniudhi yaani baada ya MC kuanza kuwaita wagombea wa ubunge wa Dar es Salaam ili waje kuwasalimia wananchi, TBC ikaanza kukata matangazo na kurejesha studio kwa kisingizio cha kuchambua mawazo ya wazungumzaji. Hali hiyo imeanza mara baada ya mgombea wa ubunge wa jimbo la Ilala kuanza kutema cheche zake.

Nimevumilia wachambue na ikafikia wakati mtangazaji akaturudisha tena pale Zakhiem lakini baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA kuanza kuzungumza eti wakakata tena na kuweka sauti zao watangazaji utadhani sisi tulikuwa tuna shida na uchambuzi wao.

Kitendo hiki kimenikera hadi nikaamua kuzima TV. Swali langu kwenu TBC, kama mlikuwa hamtaki kuonesha matangazo ni kwa nini mmerusha? Kama mnajua kwamba CHADEMA wanatoa maneno machafu (kwa mujibu wenu) ya nini kurusha vipande vipande? Mbona viongozi wa CHADEMA wameongea maneno ya kawaida tu, au ndiyo kusema mmepewa order kutoka juu?

Tanzania Broadcasting Corporation mnapaswa kubadilika na mkumbuke kuwa ninyi ni watendaji wa chombo cha Taifa. Kukata matangazo nyeti kama hayo ni kutunyima Watanzania haki yetu ya msingi ya kupata habari. Kumbukeni kuwa mishahara yenu na vifaa vyote mnavyovitumia vimetokana na kodi za Watanzania bila kujali itikadi zao za vyama. Huu mchezo waliufanya ITV lakini leo bado TBC mnaendeleza. Binafsi nimeumia sana kwa kitendo hiki na mnafanya Watanzania tuzidi kuwapuuza kabisa.

Huu ni wakati wa uchaguzi mkuu kwa taifa hivyo ni bora mkaacha upendeleo. Haya ndiyo mambo yanayotutia hasira watu na kuanza kuwachukia bila sababu. Acheni watu wazungumzie maana hata sisi Watanzania tunazo akili za kuchambua mambo, kama mtu atatema pumba tutampuuza na mtu akisema ya kweli, tutayafuata.

Uchambuzi wenu studio mngeufanya baada ya mkutano wao kufungwa na sio kutonesha picha tu huku mkiweka sauti zenu zisikike. Kuna maisha baada ya uchunguzi, kuweni makini sana ninyi watumishi.

Am out.
 
Hata wakiwa na online TV bado Watanzania wengi hawawezi kutazama kule kama ilivyo kwa televisheni ya taifa.
Bado hawawezi kukwepa lawama,lazima ukitaka kushika Dola,nimuhimu kuwa na strateji za kuwafikia watu wako.....hata kumiliki kituo chao kabisa,siyo lazima tivi hata redio tu......
 
Habari wakuu,

Leo tarehe 28 Agosti, ilikuwa ni siku rasmi ya ufunguzi wa kampeni za uchaguzi kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika jiji la Dar es Salaam. Kampeni zimeanza jioni katika uwanja wa Zakhiem-Mbagala.

Kwa sisi tulio mbali na jiji la Dar es Salaam, kiu kubwa ilikuwa ni kupata matangazo ya moja kwa moja yakionesha tukio zima la ufunguzi wa kampeni hizo ili kusikiliza sera za wagombea na kuwapima kimaono. Katika pitia pitia channel kadhaa za hapa nchini, kwa bahati nzuri nikaweka TBC1 na nimefurahi sana kuona wakirusha live tukio lile.

Kitu kilichoniudhi yaani baada ya MC kuanza kuwaita wagombea wa ubunge wa Dar es Salaam ili waje kuwasalimia wananchi, TBC ikaanza kukata matangazo na kurejesha studio kwa kisingizio cha kuchambua mawazo ya wazungumzaji. Hali hiyo imeanza mara baada ya mgombea wa ubunge wa jimbo la Ilala kuanza kutema cheche zake.

Nimevumilia wachambue na ikafikia wakati mtangazaji akaturudisha tena pale Zakhiem lakini baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA kuanza kuzungumza eti wakakata tena na kuweka sauti zao watangazaji utadhani sisi tulikuwa tuna shida na uchambuzi wao.

Kitendo hiki kimenikera hadi nikaamua kuzima TV. Swali langu kwenu TBC, kama mlikuwa hamtaki kuonesha matangazo ni kwa nini mmerusha? Kama mnajua kwamba CHADEMA wanatoa maneno machafu (kwa mujibu wenu) ya nini kurusha vipande vipande? Mbona viongozi wa CHADEMA wameongea maneno ya kawaida tu, au ndiyo kusema mmepewa order kutoka juu?

Tanzania Broadcasting Corporation mnapaswa kubadilika na mkumbuke kuwa ninyi ni watendaji wa chombo cha Taifa. Kukata matangazo nyeti kama hayo ni kutunyima Watanzania haki yetu ya msingi ya kupata habari. Kumbukeni kuwa mishahara yenu na vifaa vyote mnavyovitumia vimetokana na kodi za Watanzania bila kujali itikadi zao za vyama. Huu mchezo waliufanya ITV lakini leo bado TBC mnaendeleza. Binafsi nimeumia sana kwa kitendo hiki na mnafanya Watanzania tuzidi kuwapuuza kabisa.

Huu ni wakati wa uchaguzi mkuu kwa taifa hivyo ni bora mkaacha upendeleo. Haya ndiyo mambo yanayotutia hasira watu na kuanza kuwachukia bila sababu. Acheni watu wazungumzie maana hata sisi Watanzania tunazo akili za kuchambua mambo, kama mtu atatema pumba tutampuuza na mtu akisema ya kweli, tutayafuata.

Uchambuzi wenu studio mngeufanya baada ya mkutano wao kufungwa na sio kutonesha picha tu huku mkiweka sauti zenu zisikike. Kuna maisha baada ya uchunguzi, kuweni makini sana ninyi watumishi.

Am out.
Watanzania wote wanaangalia star TV,itv ,BBC na Azam TV. Huko kulikobakia hakuna network
 
Wapigwe tu, hamna namna, tumeshawachoka
 
Back
Top Bottom