TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

Ndugu WanaJF,

Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa picha na ubunifu wa vipindi.

Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.

Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.

Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.

Karibuni sana.
TBC ni kama ileeee KBC ya Moi.. Sema tofauti KBC was 90's & TBC sasa.. Bad!
 
Jamani nawaomba wadau hiii taarifa mnisaidie imfikie Mkurugenzi wa TBC ,nimesikitika kuona kwenye taarifa Ya habari Ya kimataifa kwenye tbc iliyohusisha habari Ya Mahakama Ya weingereza kuhusu kesi iliyokuwa inamhusisha waziri mkuu wa weingereza kusitisha bunge kwa ajiri Ya breixt Mtangazaji anadanganya usiku kweupeeee eti Mtangazaji anasema kuwa Mahakama hiyo imempa ushindi waziri mkuu, mbaya zaid Mtangazaji ameifafanua hiyo kesi kuwa Mahakama imekubali kuwa waziri mkuu alikuwa Sahihi kuiondoa weingereza kwenye mkataba wa breixt pasipo makubaliano, duuuu Mkurugenzi mtafute huyo aliesoma hiyo taaarifa haraka ajieleze hii ni television Ya taifa mtu kudanganya hivyo ni kosa kubwa mno hii tbc hata rais anaisikiliza

Nikuwa Mahakama imesema kuwa waziri mkuu alimdanganya malikia hivyo alivunja sheria kustisha bunge na tiyari serikali Ya wengereza imesema itakata rufaaa sio Kama tbc ilivyotangaza mmemaaanika jamani huyo alietangaza kadanganya
 
Mimi nawapongeza sana TBC kwa habari nzuri tatizo lao kubwa kutoa habari za upande mmoja hata kama kuja habari za vyama vingine kutoka kwake kwa tabu sana wao wameelemea ccm tu wakati hiki ni chombo cha taifa cha watanzania wote.
 
Acheni kutumika kisiasa! Tunashindwa kuwelewa kama nyie ni Television ya Taifa au tawi la chama?
Ubora wa picha ni sifuri kabisa!
Nchi hii imejaa vijana zaidi ya 70% nyie asilimia 80 ya vipindi vyenu ni vya kizee!
Mnashindwa hata kuonesha mechi ya Taifa stars mmekalia ziara za viongozi wa chama wakitembelea matawi sijui kigoma gani huko!
Mmetangaza kufunga mitambo mipya ya kisasa na picha ndo kabisa zimerudi zile za kiwango cha chini kabisa!
Subirini na wengine wanakuja na mjiandae kwa POVU ZAIDI

Usijali, Mheshimiwa sasa haitaji watu wanaojipendekeza, watanyoshwa tu!
 
Onyesheni mechi za ligi kuu Tanzania. Kwani platform yenu ni kubwa. Tungependa kuona local talents.Sijui sheria zikoje maana nasikia Azam anaonyesha
 
Mm ningeshauri mjitenge na upendeleo wa kisiasa vyama vyote ni vya tanzania mjitoe kwenye biasness ya uccm TBC ni ya watanzania wote na si ya Chama kingine mpende kuutangaza ukweli hata kama haumfuraishi mtukufu flani la mwisho ni muwe na utaratibu wa kuweka records na kuzifuatilia especially za ahadi za uchunguzi unaendelea tutawafahamisha za jeshi la polisi
 
machinga smart huyu dogo sijui kwamba hata alisoma, anauliza maswali ya kipuuzi kabisa.
wanauliza swali lilelile tuuu. "nini mchango wa mwalimu nyerere katika utalii" liliulizwa mwakajana na mwaka huu pia
Hamna weledi kabisa
 
mpuuzi wewe kodi unalipa wewe na huyo kichaa wako tu. tunaangalia tukiwa kwenye ofisi za wajinga kama wewe
Mtu akikuuliza kwa ustaarabu basi mjibu kistaarabu,hakuna haja ya kutupiana matusi.
Next time you gonna suffer de consequences of your immatured response.
 
Back
Top Bottom