TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

Matangazo ya TBC1ya kipindi cha HADUBINI ya tarehe 13/04/2019 saa 2 usiku hayakuandaliwa vizuri kwa sababu sauti ya mtangazaji ilikuwa mbaya mno na ilikuwa haisikiki vizuri.Pamoja na kwamba kipindi kilikuwa kizuri sana kilichohusu nyumba ya ghorofa mbili iliotelekezwa na mzungu.Watu wengine wote waliokuwa wanazungumza sauti zao zilikuwa zinasikika vizuri.Tatiza la sauti mbaya na kutosikika vizuri liliendelea hadi mwisho wa kipindi kana kwamba fundi mitambo wa TBC 1 hakwepo na hakuona dosara hiyo iliokuwa wazi kabisa.Wahusika pia hawakuomba msamaha kwa Watanzania kutokana na tatizo hilo. Matatizo mengi ya TBC pengine hayafanyiwi maboresho kwa sababu pengine wahusika wanajua wao wanafanyakazi kwa ufanisi mkubwa wakati sio sawa.Kumekwepo na malalamiko mengi sana kuhusu chaneli mpya Tanzania Safari inayoonesha wanyama wetu na utamaduni wa makabila mbali mbali. Malalamiko hayo yanahusu kurudia rudia vipindi vile vile kwa muda mwingi.Yapo makabila mengi na utamaduni wao na iko mikanda mingi ya wanyama lakini TBC wameng'ang'ania ile ile kila siku.Kila siku tunaona wajukuu wa Mkwawa na kabila la Wahzabi na nyumbu. Hivi hakuna hata mtu mmoja wa TBC anaepitia maoni ya wadau mitandaoni ili waweze kuyafanyia maboresho?? Hakika watu wamechoka sana kuangalia marudio ya vipindi.Wahusika tuelezezeni kuna shida gani inawasibu na maandalizi ya vipindi vyenu.Sasa watu wamehamia chaneli zingine za wanyama ambazo nazo nyingi zinatoka mbuga za wanyama wa Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie mko kwanzia uhuru na bado mnadai hamna uzoefu, steshen zingine zimekuja juzi tu na zinauzoefu tayari, kilichoshindikana kuota na mvua umande hautoweza,
 
Wengi hapo juu mmeishia kueanyuka na kuonyesha hasira zenu...Naamini jamaa wa TBC wanatakiwa kusoma yote katikati ya maneno makali hayo hayo ya wanabodi ili wachukue points humo ndani.

Lakini la pili TBC mngefanya research nchi zingine za Afrika wao wana deal vipi na nguvu ya Vyama tawala?? ili muwe na base ya maamuzi yenu maana TBC ni waajiriwa wa Umma wanafuata maelekezo tu kwasababu budget na kuteuliwa wanateuliwa na wale wako madarakani ambao ni ccm ...

Kingine TBC igeni ya Tido hata yeye aliikuta hoi taabani akaibadili kuwa bonge la Media House ghafla wakamtoa...Ayub ni mtu anajua mambo ana uzoefu ila nadhani mfumo haumruhusu kutiririka na wote mnasema hapa Afrika ukiwa na chakula mdomoni usiongee...nae katulia anamsosi mdomoni.

TBC watu wengi hasa kundi la Vijana haliwakubali kabida pamoja vijana wetu nao wanapenda mambo rahisi lakini badilikeni .
 
Toa changamoto wafanyaje ili waboreshe sio kulalamika tuu,hivi wakati wa tido kipi kikubwa kilikuwepo haswa manake mie sikukiona hasa sema wewe
 
Mulikuja kuindeleza hii tasnia kwa manufaa yenu na mkufurahisha boss wenu wakati sisi ndio walipa kodi hapo harafu mwambie mkurugenzi wenu akumbuke familia yake aliotoka kuzaliwa japo wote ni binadamu tunamakosa
 
TBC ni janga kubwa sana kwa kweli...kuanzia signals , mpangilio wa vipindi , watangazaji kama wamechongwa hawana mvuto hata kidogo...kunaweza kuwa na breking news nyie mmeng'ang'ania mavipindi yenu ya ajabu ajabu unless ihusiane na CCM na Jiwe ndiyyo mtarusha live.....hapo panatakiwa reshuffle ya maana....manake sasa kama mnapitwa na watu kama Wasafi TV ,Clouds TV ambao hawaangalii sana n mavyeti na uzoefu wa miaka 30 sijui...ni ubunifu na vipaji kwanza....sijui mtaanzia wapi kwa kweli
 
Ndugu WanaJF,

Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa picha na ubunifu wa vipindi.

Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.

Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.

Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.

Karibuni sana.

Badilishweni tabia zenu kabla hatujaanza kushauri
 
Hapana mkuu wala sikuchukulii poa. Najaribu tu kusisitiza tuweke mkazo kwenye kushauri cha kufanya badala ya kuishia kutaja changamoto ambazo zinafahamika.

Yaani kama una kiu, kulalamika tu hakutoondoa kiu Bali kutafuta maji na kuyanywa.

So, kutaja tu matatizo ya TBC hakutoyaondoa bali kupendekeza na solution ndio kutasaidia kuboresha.

Mfano kwenye hili la ubora umeeleza vizuri. Nakuunga mkono. But nadhani ndicho kinachofanyika huko TBC tangu juzi. Ni imani yangu tutaona mabadiliko ktk eneo hilo hivi karibuni.

Tuangazie kwenye vipindi sasa..
Hivi nikitaja changamoto si ndio nimeshauri nini kifanyike, hata kama sio moja kwa moja. Mfano nikisema ubora wa picha ni mbovu si ndo namaanisha mrekebishe ubora wa picha. Au mpaka niseme mboreshe kwa namna gani? Hiyo si ndio kazi yenu? Mi ntajuaje wakati sina utalaamu huo? Mimi kama mtazamaji nitakachoona ni ubora wa picha, mbovu au nzuri. Nini kinafanyika ili picha iwe nzuri sio kazi yangu!
 
Mi napmba nijue, Ni lini mtaboresha mitambo yenu kwa wneo la kilolo milima ya udzungwa; ngangange, bomalangombe, masisiwe, udegenda na vijiji vingie ili tuwapate vizuri km mnavyojinadi kuwa niliondokewa ninyi ni bora!?
 
Boresha kwanza mwandiko wako kabla hujaboreshewa huduma.
 
TBC ni janga kubwa sana kwa kweli...kuanzia signals , mpangilio wa vipindi , watangazaji kama wamechongwa hawana mvuto hata kidogo...kunaweza kuwa na breking news nyie mmeng'ang'ania mavipindi yenu ya ajabu ajabu unless ihusiane na CCM na Jiwe ndiyyo mtarusha live.....hapo panatakiwa reshuffle ya maana....manake sasa kama mnapitwa na watu kama Wasafi TV ,Clouds TV ambao hawaangalii sana n mavyeti na uzoefu wa miaka 30 sijui...ni ubunifu na vipaji kwanza....sijui mtaanzia wapi kwa kweli
Unataka kufananisha hizo Chanel na TV ya serikali? Harafu wewe hizo Chanel zina kipi cha ziada?
 
Ndugu WanaJF,

Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa picha na ubunifu wa vipindi.

Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.

Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.

Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.

Karibuni sana.
Naomba Ushauri wangu niandike kwa Herufi Kubwa,,

[/b]BORESHENI UBORA WA PICHA[/b]
 
UBORA WA PICHA MBOVU MNOOOOOO, MNAKERA KODI ZETU ZOTE HZO PICHA MBOVU
 
Back
Top Bottom