TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

Chaneli yenu mpya ya "Tanzania Safari" iwepo katika Ving'amuzi vyote. Itawaongezea pointi nyingi mkiisimamia vizuri.
...
Tuambiane mapema nani anamiliki hii kitu?¿¡!
Tunaambiwa mpaka taratibu za kisheria zifuatwe.
Wanatakiwa warushe zile tv kama fta, wametikisa. Minara na ofisi zao ni gharama ya nchi.
Nakumbuka waliplug state of art mobile tv truck kama la zim.
Hiki kweli ni kiziba mdomo tosha, kawaida kuna mengine na yajayo tunayasubiri.
...
 
Hovyo kabisa, Badala ya kumtafuta Tido Muhaondo awape ushauri, mmemfungulia kesi, yaani hovyo, namaanisha hovyo kwa kweli, hovyo mara hovyo, mmegeuka tawi la CCM, Yaan namuangalia Ryoba mpaka namshangaa, utadhani shuleni alienda kusomea ujinga
du!pole kwa hasira
 
Mim hata sielewi ni tv ya taifa au ya ccm maana kila kitu kinachoonyeshwa ni ccm hivi, kama ni tv ya taifa kwanini mnaonyesha mambo ya ccm tu mbona kuna mambo mengi yaani taarifa za habari zote huwezi ona taarifa za vyama vingine ok tuachane na vyama siku ya uhuru sikuona hata maandishi yanayoonyesha kuuenzi uhuru niliona kwenye tv nyingine ila tv ya taifa hata maandishi kuashilia ni siku ya uhuru hamna ila kama hambadiliki sizan kama mtapata watazamaji wengi zaidi ya wanachama tu.
 
Kipindi cha kitimoto kirejeshwe, Analetwa studio waziri, naibu waziri, katibu mkuu wake na wakirugenzi. Wanapigwa maswali live kutoka kwa wananchi. Hiyo itaongeza uwajibikaji wa viongozi na pia kuzijua kero za wananchi.
 
Suala la ubora wa picha za TBC ni janga la taifa. Sijui kwa nini TBC hamtaki kujifunza kwa majirani kama Rwanda TV na Kenya. Kwanini mnang'ang'ana kuinvest kwenye wide coverage badala ya kuivest kwenye ubora (quality)? Mmeshafanya survey kuona ni kwa kiwango gani waangaliaji wa TV wanaangalia matangazo yenu? Unajua hata content isipokuwa bora sana, watu wanaweza kuvutiwa na quality.

Msishangae Kenya wakawaiga kuanzisha TV channel ya Tourism na yao ikawa na quality, audience na tija kubwa kuliko ninyi mlioanza kuja na hili wazo!!!

Lingine TBC wana tabia moja very annoying ya kuongeza sauti kwa kiwango kikubwa sana kwenye matangazo ya biashara (commercials). Kwa watu tunaojua TV huu ni ushamba mmoja mkubwa sana. Kama TCRA hawana kanuni tafadhali waziweke kudhibiti hii tabia.

Nilikuwa TZ kwa mwezi mmoja: Ukiwa DSTV ukitaka kwenda TBC shurti uwe na remote control yako mkononi maana kila wakibadili toka matangazo ya kawaida kwenda commercials wanaongeza sauti kwa kiwango kikubwa sana.

Hii tabia vile vile stations nyingine wanayo ila hawazidishi sana sauti kama TBC!!! Kwa hiyo, hoja yangu si kwamba waache bali wasiongeze sauti kwa kiwango kikubwa saana kama wafanyavyo sasa. Sababu watazamaji wa TBC na TZ kwa ujumla hawana 'TV Sound Regulators.' Na sauti ikiwa kubwa sana, mtu unalazimika kuzima kabisa sauti (mute) kwenye remote control kwa hasira!!!. Kwa maana hiyo, hata hiyo commercial inakosa tija!!!

Ili kudhibiti hii tabia TCRA wanaweza kujifunza kutoka Marekani: The CALM (Commercial Advertisement Loudness Mitigation) Act.
 
Naangalia matangazo ya moja kwa moja IKULU Kwa kweli TBC mnaaibisha sana! mlisema mnabadili mitambo kuwa ya kisasa! Yaani ni Hovyo kabisa hasa upande wa SAUTI mara ipande mara ishuke! video kama za TECNO elfu 60

khaaaa huku kuna shida sana
 
Mkuu umetoa wazozuri but inaitajika tutambue kuwa TBC nichanel ya taifa so lazima ijitahidi kufata na kutunza misingi ya habari na heshima kiujumla vile vile tusije kutegemea kwamba TBC itakuja kuwa Chanel pendwa km ilivyo kuwa clouds au eatv coz TBC haiwezi kutangaza habari zinazo tupendeza sisi vijana kwamfano Leo tunataka kusikia habari kuhusu skendo za mastaa ambazo kwaasilimia kubwa zinaibomoa jamii na kuharibu tamaduni zetu km watanzania, na hata tukiangalia hizo Chanel tunazo zisifia vipindi vyake pendwa na vinavyo sifika nivipindi ambavyo nivigumu Sana kusikika katika Chanel km TBC.
kuutwa mmikalia jiwee jiwee uzinduzi live mbona bunge hamuonyesh live

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TBC mmemezwa na habari za upendeleo za ccm hata taarifa ya mjumbe wa mtaa wa ccm mnatangaza ktk taarifa zenu lakini hamuwezi kutangaza taarifa ya maalim seif Sharif hamad au taarifa za zito kabwe akingea na wanachama wake !
Mko tayari kutoa taarifa tu za vyama vya siasa pale wanapokuwa mahakamani au wakipelekwa mahabusu huu ni udhaifu mkumbuke asilimia 60 ya waTz ni vijana tena waliozaliwa wakati nchi ikiwa ktk mfumo wa vyama vingi kwa hiyo wanahitaji taarifa mseto toka vyama vyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
binafsi nawashauri mjipange upya tu maana hata ile tbc 2 haiko vizuri sijui mliianzisha kwa mallengo gani hasa ? vipindi vyeenu havina mvuto, bashasha
 
Back
Top Bottom