Coaster2015
JF-Expert Member
- Aug 21, 2018
- 2,594
- 2,716
Huwezi kuacha kumlaumu rais kwenye failure ya Tbc kwani ni kweli ndie anaechangia kufanya mambo yawe mabaya zaidi, hata ukimuweka kiongozi gani kuisimamia Tbc haitaweza kujiboresha chini ya rais huyu kwa sababu yeye hataki kuona watu wengine wanasifiwa isipokuwa yeye tu na ccm yake, sasa haya makosa makubwa ya rais kwani anachokitaka ndicho kinachoidhoofisha tbc, Anthony Dialo alijaribu kuwapa Uhuru na Nafasi kubwa wapinzani kwenye kituo chake cha StarTV muulize alichofanyiwa na ccmHapo naomba kutofautiana na wewe. Kwa Rais aliepo madarakani swala ni kujenga hoja baada ya kujitathmini. Taasisi kama TBC imezeeka kimuundo na kimfumo. Kwa kutizama tu vipindi vyao unajua jinsi wanavyoplan. In incremental. Ya mwaka ujao ni ya mwaka jana badilisha hapa na pale ...maisha yasonge. TBC inahitaji total overthaul. Unapotafuta mkuu wa taasisi na vitengo unatafuta mtu mwenye vision na uwezo wa kusimamia vision. Nani asieikumbuka National Housing ilivyobadilika baada ya kupata viongozi sahihi? CRDB Je, nk. Taasisi zimekuwa tamu mpaka watu wameanza kupigana vikumbo kwa fitna.
Tubadili mbinu jinsi ya kutafuta CEOs na waachwe watekeleze vision zao. Political interference iwe pia tamed.
Utamlaumu Rais kama kweli anaingilia kazi nzuri. Lakini kama kazi ni mbaya unamtegemea akae kimya?
Tuwasaidie TBC kwa kuwaeleza njia na mbinu sahihi za kupitia watoke hapo walipo maana kweli wana hali mbaya.
Its too sad to see our cash cow being mismanaged.
Ng'ombe huyo alipaswa kutoa lita 20 lakini anayoa lita 5 japo anakula majani yaleyale.