TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
918
1,994
Ndugu WanaJF,

Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa picha na ubunifu wa vipindi.

Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.

Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.

Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.

Karibuni sana.
 
Acheni kutumika kisiasa! Tunashindwa kuwelewa kama nyie ni Television ya Taifa au tawi la chama?
Ubora wa picha ni sifuri kabisa!
Nchi hii imejaa vijana zaidi ya 70% nyie asilimia 80 ya vipindi vyenu ni vya kizee!
Mnashindwa hata kuonesha mechi ya Taifa stars mmekalia ziara za viongozi wa chama wakitembelea matawi sijui kigoma gani huko!
Mmetangaza kufunga mitambo mipya ya kisasa na picha ndo kabisa zimerudi zile za kiwango cha chini kabisa!
Subirini na wengine wanakuja na mjiandae kwa POVU ZAIDI
 
Utangazaji ni kipaji na sio mavyeti tu..hawashangai clouds media wanaendelea kuwa relevant kwa kiasi fulani kutokana na kuweka watu wenye vipaji na sio tu degree ya mass communication na journalism..

Sehemu ukishajazaa wazee wengi hata ubunifu unakuwa hamna..refer taasisi nyingi za serikali kama Ttcl na nyingine..
 
1.Acheni u ccm unawezaje kurusha ziara,mikutano ya ccm halafu bunge usionyeshe live?
2.Mbona habari za vyama,viongozi wa upinzani hamzionyeshi?
3.Kuwe na taarifa ya habari za uchunguzi wa kero za wananchi siyo kuonyesha mikutano ya viongozi.
4.Taarifa za Habari ziwe kwa kiingereza na kiswahili.
5.Mipira michezo jitahidini sana kuonyesha live
6.Kuwe na vipindi vya kilimo cha kisasa teknolojia mpya uzalishaji katika viwanda kero zao
 
Acheni kutumika kisiasa! Tunashindwa kuwelewa kama nyie ni Television ya Taifa au tawi la chama?
Ubora wa picha ni sifuri kabisa!
Nchi hii imejaa vijana zaidi ya 70% nyie asilimia 80 ya vipindi vyenu ni vya kizee!
Mnashindwa hata kuonesha mechi ya Taifa stars mmekalia ziara za viongozi wa chama wakitembelea matawi sijui kigoma gani huko!
Mmetangaza kufunga mitambo mipya ya kisasa na picha ndo kabisa zimerudi zile za kiwango cha chini kabisa!
Subirini na wengine wanakuja na mjiandae kwa POVU ZAIDI
Maoni yangu ni haya
 
Back
Top Bottom