Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 918
- 1,994
Ndugu WanaJF,
Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa picha na ubunifu wa vipindi.
Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.
Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.
Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.
Karibuni sana.