TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

TBC mpaka iwe mpya sio rahisi.
1. Mwandaaji na aina ya vipindi ni vya kizee mno. Ubunifu ni zero.
2. Mnavaa kama madereva na sio watangazaji. Mnekukula mmenenepeana haswa wanawake ni vipipa. Hao rudisha nyuma kuandaa na kuongoza vipindi. Eleweni kutangaza kwenye tv ni zaidi ya kazi ya PR. Muonekano ndio branding. Get people with best voice and appearence plus brains. WAPO TELE.
3. Hamjaweza tumia teknologia ipasavyo. Quality ya video zenu inasikitisha. TV ya Taifa? No way. Mnashindwaje na madogo kama ayo, itv nk ?
4. Wekeni channels tofauti. Say TBC 1 huko wekeni watu wa serikali na programme za kuisifu serikali. Fine. TBC 2 ya biashara na programme zilizochangamka za vijana, kisasa, nk
TBC 3 say International hii ni ya utalii na kwa kiingereza. Huko unaiuza Tanzania duniani na sera ya viwanda na ipatikane free duniani kote na balozi zetu na airport zote na portal zote kubwa. Weka vivutio, mahoteli, mbuga, na quality ya picha iwe ya kimataifa.
5. Hiyo serikali mtandao ionekane kimataifa. Mambo ya passport, viza, uwekezaji na fursa. Wawepo watu wanaojua lugha na sio kiingereza cha kihaya.
Nimesoma commengts za watu wengi humu ndani hawaangalii TBC na kuanza kujiropokea tu. Kwa aarifa yako waambieni vijana wenzenu wanaotafuta fursa sasa TV yao iwe TBC wasikae kumuangalkia Dimind na wendinea wasika lie Ndombolo badala ya kutafuta fursa. TBC imeanza kuboreka saaana! Hivyo toeni constructive critisimm. Angalau MDAY huyu ametoa na suggestion.
 
Vipindi vyao vingi havina mvuto kwa mtazamaji, wao kazi kusifia tuu, yaani mtu anasifiwa mpaka unaamua kuzima tv
Tanzania tuna matatizo mengi mno, lakini kwenye taarifa ya habari huoni wakiripoti, wao kusifia tuu mmekua kama nyamwazi aisee mnatia hasira sana
 
naomba TBC mzingatie kuweka majina ya watu mnaowahoji kwenye Taarifa zenu mnazoturushia.

Unakuta mnachukua taarifa Fulani halafu mnayemhoji/mnaowahoji hamuweki majina wala tittle zao kama wafanyavyo ITV.

Hili linatukera sana sisi wafuatiliaji wa TBC.

Kama sijaeleweka, niambieni hamjaelewa wapi nifafanue zaidi.

Ni kero mno hii
 
Katika televisheni yenye kuboa ni yenu! Mnakumbusha TV za kichina enzi za Mao the tung!. Mnasifia tu hamuoneshi changamoto nyingine za upande wa pili. Mfano Hivi hiyo TBC ni ya chama tawala?. Je mkionesha Sera za vyama vingine mtaugua? Acheni ushamba wa karne ya 47! Hata Nyerere alipinga wazo la kumsifia kizushi nyie sijui mmepata Wapi Hii tabia. Kifupi hamfai kwa kuwa hamvutii
 
Tbc mnaegemea mlengo fulani ndio maana watu wanalalamika mimi tangu chanel zimekatwa na kubakia tbc nimehamia Dstv kwa ajili ya michezo pekee kwaherini nitarejea yatakapo fanyika marekebisho makubwa
 
1. Rekebisheni volume (ukubwa wa sauti) za matangazo ya biashara.
Mtu unasikiliza taarifa ya habari kwa sauti ya kawaida, mara linatokea tangazo la tigo, volume iko juuuuuu, tunanza kutafuta remote ili kupunguza sauti. Tangazo likiisha inabidi kupandisha tena.

2. Usomaji wa habari za kimataifa:
Someni kwa vituo. Sio mnasoma kama mnaimba.
Mnashindwa hata kuchomekea maneno ya kuunganisha/kutenganisha habari kiasi kuwa habari ya Uturuki haijaisha vizuri, tayari inakuwa imeunganishwa na habari ya Marekani as if ni taarifa moja.

3. Ukamilifu wa habari.
Kamilisheni taarifa. Sio mnajiunga na mtangazaji aliye nje ya studio anaeleza kidogo na kabla taarifa haijaeleweka vizuri, mnakatisha.

4. Nitarudi kesho nikiwa kwenye computer.
Kwa habari za Kimataifa wana download za aljazeer, CNN nk sasa sijui kama wataweza kutenganisha
 
bado hawawez kubalance Sauti ... PIA mtangazaji anasema Tupate taarifa Kamili, wanabak wameganda km Dakika nzima... Hakuna ubora kabisa. Km mitambo feki wekeni mipya ...mmezubaa Sana had huruma
 
Mnaegemea kwenye chama cha jiwe
Mnaacha vyama Vingine
Hiyo ni double standard
Ndugu WanaJF,

Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa vipindi na ubunifu.

Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.

Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.

Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.

Karibuni sana.
 
Kila ukiwasha tv unakutana neno safari ya dodoma hiyo tbc siangalii mimi siielewi,chaneli inasifia vitu vya ajabu ajabu habar yenyewe haina mvuto
 
hiyo channel inapatikana wapi, kwenye king'muzi changu DSTV&AZAM HAMNA KABISA.
Lakini ni bora tu niendelee kutazama UBC
 
Siku mkiaza kutangaza habari zenu kama TV ya taifa na si kama ya 'sisiemu', nishtueni.
Mlipoamua kutoa station zingine kwenye DSTV ndo ilikua mara yangu ya mwisho kuitizama TBC. Infact nilikua naangalia TBC zinapoanza habari za kimataifa hadi kwenye michezo tu. So, sijui nini kinaendelea TBC sku hizi. Rudisheni station zingine za local kwenye ving'amuzi vyetu pendwa tafadhalini sana.
 
TBC ni uchafu.....cha msingi ijitenge na serikali ya CCM ijiendeshe hasa kwa kutokuingiliwa...

TBC mnatakiwa kumrudisha Tido Mhando..

Msipomrudisha mtafeli kila siku!
 
Back
Top Bottom