TBC mnachokifanya ni ujambazi!

moghasa

JF-Expert Member
May 7, 2013
1,084
1,251
Umofia kwenu Jamiination!

Leo baada ya kuishiwa kifurushi cha Azam sikuwa na namna badala yake ilinibidi niangalie TBC siku nzima yaani mpaka muda huu naandika hapa! (Simba kakosa nyama)
Katika kodoa kodoa zangu mbele ya uchawi huu wa kizungu Mara kikaanza kipindi kilichoenda kwa jina la "Utamaduni Wetu" . Ndani ya kipindi hicho anaonekana Mzee aliyejitambulisha kwa jina la Mwalko mpiga malimba maarufu kama alivyoonekana ndani ya kipindi, mpaka hapo sikuwa na shida, shida ni hii.

Haukupita muda yakaonekana matangazo ya kibiashara yanayohusu tamasha sijui "Club Rahaleo Show" wanamtumia Mzee Mwalko, tangazo linaanza kwa kusema "... Je unakipaji kama hiki ( anaoneshwa Mzee Mwalko akipiga malimba na kuimba) kama jibu ni ndiyo basi..." Tangazo linaendelea kwa mbwembwe kuwakaribisha watu kuchukua fomu za kujiunga na usaili wa hilo shindano.

Najua jamiination inawatu weledi, wataalamu na wajuvi wa mambo haya ya matangazo na nikiwa na imani kuwa huyu Mzee hajanufaika kwa uzoefu wangu wa miaka 30 ndani ya taifa hili la kiswahili, naomba tuelimishane kama Mzee anapaswa kudai chake ama la!

Nb. Nimeshindwa kuweka caption kwani wakati wa tangazo TV haikuwa na storage device ili nichukue picha ! Nikiona tena ntaweka kwani Niko standby na remote yangu mkononi.

Nawasilisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom