TBC mna siri gani na Muhongo?

MTENDAHAKI

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
4,013
1,443
Hivi TBC Kama chombo cha umma kujaribu kumpigia debe Muhongo "eti wananchi wa Lindi wamepeleka ombi maalum kwa JK" ni sawa?

Naomba TBC wajue Kuwa wananchi hawako Lindi tu hata Dsm kuna watanzania, Moro kuna watanzania, Mbeya na kwingineko kote kuna watanzania na wengi wetu tunaunga mkono maazimio ya bunge!

Hakuna maana yoyote kwa chombo cha umma kumtetea mtu mmoja mtuhumiwa wa kutumia vibaya madaraka.
 
Jamaa wanamwaga PESA kila mahali kumlinda Muhongo jamaa anaonesha yupo tayari kufa kiafisa na tai shingoni....
Kinachomsumbua huyo Prof ni hiyo rank ya shule kwani anaona fedheha kuonekana Prof ameshindwa, na hii ni hulka ya wasomi wengi kutokubali kwamba wamefanya makosa.
 
Kuna gazeti linaitwa TAZAMA,nalo sijui lina ubia gani na Muongo,hata kabla ya escrow limekuwa mstari wa mbele kumpaisha jamaa.
Sijui ndio presidential material wa kulinda maslahi ya Msoga huyu?maana anapaishwa kweli.
 
TAZAMA ni gazeti la Msaka tonge mmoja ambaye ni kada wa magamba. Alitegemea kuingia kwake ccm kungempa ulaji wa kuwa mkuu wa kitengo cha habari. Jamaa wakamstukia kwamba hawawezi kumwingiza kwenye mgao wa keki yao wakamtelekeza. Anachofanya sasa hivi ni kama kupiga makelele akiwa anazama ili wamwone na kumtupia japo makombo.
Gazeti halitoi hata nakala 50 kwa wiki, na hakuna hata moja inayouzika unategemea nini?
 
TBC wanajisahau sana kiasi cha kushindwa kuelewa kuwa wanajiendesha kwa kodi zetu.... Hizo fedha za UFISADI walizohongwa soon zitaisha ...
 
Hivi TBC Kama chombo cha umma kujaribu kumpigia debe Muhongo "eti wananchi wa Lindi wamepeleka ombi maalum kwa JK" ni sawa?

Naomba TBC wajue Kuwa wananchi hawako Lindi tu hata Dsm kuna watanzania, Moro kuna watanzania, Mbeya na kwingineko kote kuna watanzania na wengi wetu tunaunga mkono maazimio ya bunge!

Hakuna maana yoyote kwa chombo cha umma kumtetea mtu mmoja mtuhumiwa wa kutumia vibaya madaraka.

Wacha wa balance Mbona ITV kutwa kumchafua
 
nchi ya wezi!!
wezi wameshika vyombo vya dola siyo vya habari tu!!
 
TBC nyinyi hamko mbinguni tupo wote Tanzania hata kama nyinyi hamdaiwi pesa za ujenzi wa maabara,pengine wazazi shemeji kaka au dada zenu wanahagaishwa na michango isiyo isha ya serikali huku Sethi,Muhongo na wenziwe wamekula keki yao.Acheni kutumika kama TISSUE za ...ni.Nchi hii inaongozwa kwa sheria na taratibu.
 
mtendahaki usiwe punguani..nenda na wewe na watu wako TBC mkazungumze kuwa munataka Profesa Muhongo ang'olewe nao watakupokea na watarusha live maoni yenu..usiwanyime watu haki yao kisa uko kundi la walewale...
Hivi TBC Kama chombo cha umma kujaribu kumpigia debe Muhongo "eti wananchi wa Lindi wamepeleka ombi maalum kwa JK" ni sawa?

Naomba TBC wajue Kuwa wananchi hawako Lindi tu hata Dsm kuna watanzania, Moro kuna watanzania, Mbeya na kwingineko kote kuna watanzania na wengi wetu tunaunga mkono maazimio ya bunge!

Hakuna maana yoyote kwa chombo cha umma kumtetea mtu mmoja mtuhumiwa wa kutumia vibaya madaraka.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom