TBC mmezidi sasa!hata hesabu ndogo inawashinda?

MWananyati

Senior Member
Feb 3, 2011
160
53
Hawa TBC saa ingine huwa nashindwa kuwaelewa. Mara kwa mara huwa nawasikia wakisema wanaonekana kwa njkia ya setelaiti hadi nchi za magharibi za marekani na ulaya n.k.
Ila inaonekana waandaaji wa taarifa ya habari hawako makini na baadhi ya vitu.
kwa mfano leo wakati wanasoma taarifa ya nauli za kigamboni wakasema kuwa watu wanalalamikia ongezeko hilo hasa upande wa maguta. Nauli yake imepanda toka 200 hadi 1800 shilingi. Waliponiacha hoi ni pale waliposema hili ongezeko ni la asilimia 80! tena wamerudia mara mbili, na hata mtangazaji anaonekana kutogundua chochote.

Mie na hesabu zangu ndogo ikabidi nichukue kalam na karatasi kwa sababu sikuamini hilo ongezeko ni asilimia walizotaja ukilinganisha na ile ya abiria ambayo imeongezeka kwa asilimia 100 (toka mia 100 adi mia 200).

Ki ukweli ongezeko la maguta ni ASILIMIA 800 ya bei ya awali iliyotozwa.

TBC, Muongeze umakini mnapoandaa taarif zenu. nyie ni chombo cha serikali hivyo tunaamini/naamini mna watu wataalamu na wajuzi wa mambo ambao kwa ujumla watakua makini katika kuandaa taarifa zenu!

GALAGABAHOOOOO!
 
watu wanakimbia combi zinazohusisha math lakini unawakuta wana madiploma ya journalism makali halafu wanatangazia taifa
 
Tumeshayazoea madudu yao.Fuatilia hata yale maandishi yao yanayopita chini ya screen huwa yana makosa kibao lakini jamaa huwa wanapuyanga tu!
 
mi mwenyewe nimestuka. hata kama hawa wenzagu hsabu kwa ni ngumu wajitahd kutafta mharr wa mahesabu. kama naur ya magut imepanda toka 500 had 1800 hi ni sawa na kupanda kwa sh 1300 sa na asilimia 260. kilichofanyka si muujiza unachukua ongezeko unagawa kwa bei ya zaman na kuzidish kwa mia
 
Sasa nyie bado tu hamjaacha kuangalia chaneli hiyo. Si bora mpoteze muda wenu kuangalia ustadi wa kukata kiuno wa katuni Odeo.
 
mkuu TBC makaosa nila siku sijui hwajiandai kusoma taarifa, sijui uwezo wakitaaluma wa watangazaji na msimamizi wao ni mdogo, yaani sielewi kabisa. Nimeona nianzishe uzi wa kuweka kumbukumbu za makosa ya TBC
 
mimi ninavyo, kwa kuwa TBC ni chombo cha sirikali, na aliyepandisha nauli ni sirikali...inwezekana mtangazaji hajakosea kafanya makusudi ili kupotezea au pengine kaelekezwa na wakuu wake. Kuanzia std 1 hadi form 4 hisabati hufundishwa kwa wote waliopitia madarasa hayo, haiwezekani ktk mazingira ya kawaida akashindwa kufanya hesabu ndogo namna hiyo.
 
mkuu TBC makaosa nila siku sijui hwajiandai kusoma taarifa, sijui uwezo wakitaaluma wa watangazaji na msimamizi wao ni mdogo, yaani sielewi kabisa. Nimeona nianzishe uzi wa kuweka kumbukumbu za makosa ya TBC

Toka wamfukuze Tido hakuna kinachoendelea zaidi ya kuimba CCM
 
Sasa hesabu ndogo namna hiyo inawapa tabu, je ingekua inahusisha mambo ya Log, Sine, Hyperbolic Function, Calculus e.t.c si ndio tungekimbiana!!!!
 
kwao kila siku ni bora taarifa ya habari, hawana mda na ufanisi wala ubora wa taarifa zao..
 
mi hao cwashangai sana kwa hilo kwani kila cku wanaboronga kuanzia watangazaji wanavyotangaza mpaka maandishi yanayopita chini kwenye screen...vilevile kunamtangazaji m1 alishakiri waziwazi hajui hesabu na form 4 alipata F ya namba.
 
Back
Top Bottom