Tbc kuwatumia kina masanja kuhujumu demokrasia.

Iga

Senior Member
Dec 17, 2007
112
6
HIVI leo kina Masanja, Joti, Mpoki na wenzao wanaanza KUTUMIWA na Tanganyika Broadcastinga Corporation katika medali ya kejeli na vichekesho.

Tofauti na walivyokuwa wakiigiza katika Independent Television [Tunamuomba Mzee Mengi afanye juu chini kupata vijana wengine watundu kama kina Masanja badala yao badala ya kupoteza muda wake mahakamani] kina Masanja sasa watatumiwa na TBC kwa niaba ya kuendeleza sera na mikakati ya CCM kuhujumu demokrasia na kusambaratisha upinzani chipukizi unaoanza kuota meno ya mwanzo kabisa hapa nchini.

Wale wote wanaotaka kuona Tanzania ikiwa na vyama viwili vikubwa kama vile kulivyo Marekani anakokuhusudu sana Mtawala wetu wa sasa, yaani Democrats na Republic.

Kweutu sisi Republics ni CCM na bila shaka kama Chadema na CUF tu [achilia wapuuzi wengine wanaoutumiwa na CCM wanaojiita wapinzani] basi Democrats watapatikana.

[ Tunawaomba wazee Lipumba, Sefu, Makani na Mtei wafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha CUF na CHADEMA wanaungana ikiwezekana mwishoni mwa mwaka huu ] ili kuhimili hujuma na janja ya CCM za kupaka matope wapinzania na kuwatumia wanaotumiwa katika nchi hii katika kueneza uwongo unaoharibia vyama vya upinzani kwa kuwatumia mamluki wa upinzani wakiwemo wachungaji, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na polisi ambao hawajui kwamba wanastahili kuwajibika kwa wananchi na sio kwa CHAMA FULANI!
 
Back
Top Bottom