tanganyika yetu
Member
- Nov 23, 2011
- 45
- 17
Taarifa ya habari jana usiku saa 2 ilisema TBC watarusha tu matangazo bunge ya maswali na majibu asubuhi na yale mengine yatatafutiwa kipindi maalum. Huu utaratibu mpya ulipotangazwa bungeni na wazari mwenye dhamana UKAWA walikataa na kudai watahakikisha wananchi wanapata matangazo ya bunge live. Leo bunge linaanza tena na ni bunge la muhimu sana kwani ni la bajeti, sasa wananchi tunakosa fursa ya kuliona na kusikiliza kinachoendelea bungeni. Ukawa mnasemaje kuhusu bunge kutorushwa live? UKAWA mmeshindwa kutetea wananchi wapate haki zao za msingi kama katiba inavyodai kila mtu ana haki ya kutoa na kupata habari?