TBC kurusha LIVE Mwaka mmoja wa RC Makonda: Ayubu Rioba, kwanini usijiuzulu?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,229
116,840
Juzi nilipoona TBC1 wako 'live' kwenye sherehe ya kuadhimisha mwaka mmoja wa Paul Makonda na watu wakawa wanajiuliza inakuaje TBC1 hawaoneshi bunge live lakini wanaonesha sherehe kama hiyo nikawa najiuliza

Je Rioba yuko comfortable kabisa na hayo yote?

kama analazimishwa why asijiuzulu?

Rioba na usomi wote anakubali kutumika na sherehe za aina ile kweli?

au Rioba yule na wa sasa ni tofauti?
 
Juzi nilipoona TBC1 wako 'live' kwenye sherehe ya kuadhimisha mwaka mmoja
wa Paul Makonda na watu wakawa wanajiuliza inakuaje TBC1 hawaoneshi bunge live
but wanaonesha sherehe kama hiyo nikawa najiuliza

Je Rioba yuko comfortable kabisa na hayo yote?

kama analazimishwa why asijiuzulu?

Rioba na usomi wote anakubali kutumika na sherehe za aina ile kweli?

au Rioba yule na wa sasa ni tofauti?
Rioba mboga ya mlenda legelege
 
Rioba mwalimu makini sijui kawaje

Mtu yoyote akijiunga ccm anabadilika kabisa,on a mwakyembe

Anyway,ayoub hawezi kujibu huku anatafuna chakula mdomoni

Nimejiuliza ile heshima yoote anakubali iharibike?
 
Ashaona ugumu wa ku practise theory ambazo huwa ana zifundisha hasa kwa hapa tz. Ndi jiulize kwanini Tido Mhando aliweza ila PhD holder anashindwa?
Kilicho baki now aendelee kupiga mshahra tuu, ila kasha haribu cv yake, pia kapoteza credibility yake na mema yake yote aliyo ya fanya before.
 
tbc toka walipoonyesha taarabu wakati wa kuzama kwa meli kule zanzibar....

wakaonyesha harusi ya tajiri mmoja mhaya live.....

nilowaona ni tv ya taifa ajabu la dunia.........

pale hata aje mkurugenzi wa CNN bila kufanyiwa reform kutoka tbc ccm na kuwa broadcasting cooperation tutasubiri mpaka yesu atakaporudi.......
 
Na hii ni namna ya kutufikishia ujumbe ant bashite kua bado yupo sana, ni kama wamempa promo flani.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
tbc toka walipoonyesha taarabu wakati wa kuzama kwa melo kule zanzibar....

wakaonyesha harusi ya tajiri mmoja mhaya live.....

nilowaona ni tv ya taifa ajabu la dunia.........

Hayo mengi yalitokea kabla ya Rioba kuja
tukajua itabadilika....kumbe wapi
 
Ashaona ugumu wa ku practise theory ambazo huwa ana zifundisha hasa kwa hapa tz. Ndi jiulize kwanini Tido Mhando aliweza ila PhD holder anashindwa?
Kilicho baki now aendelee kupiga mshahra tuu, ila kasha haribu cv yake, pia kapoteza credibility yake na mema yake yote aliyo ya fanya before.

I hope atakusoma
 
TV rasmi ya Taifa/Serikali kuonesha sherehe za mkuu wa mkoa kuadhimisha mwaka mmoja wa kuwa madarakani! Nilitegemea awamu hii madaraka ni mzigo kweli kweli kumbe sivyo tulivyoaminishwa nasi tukaamini. Sherehe! Kwa lipi hasa? Na hata kama lingekuwepo kwa sheria au kanuni zipi za kiserikali kufanya sherehe? Tangu enzi za Mwl. ni juzi limetokea tukio la aina hiyo.
 
Imagine unapigiwa simu na dingi kwamba "kijana niliyependezwa nae" yupo njiani kuja studio, apewe air time ya kutosha. Unafanyaje? Mtumbua majipu hakawii kulitumbua hata usiku wa manane, ukichukulia bado kuna sintofahamu ya fake news.
 
Ndo maana tunasema ajiuzulu tu kuepusha fedheha yote hiyo
 
  • Thanks
Reactions: SDG
msilaumu bila kuhoji! kama GSM wamelipia airtime kwa nini akatae

Hata kama wamelipia ila hoja ni kuwa tu kwa heshima aliyojijengea hapo kabla angejiuzulu tu ili asizidi kuuharibu Usomi wake.

TBC haikuwa hadhi yake, yeye angeendelea tu kufundisha.

Toka alivyopata huo ulaji Makala akawa ahandiki tena na hata mitandaoni akapotea kabisa. Hii inaitwa Ukitaka Mwafrika asahau kila kitu alichokuwa anapigania hapo awali basi mpe cheo.

Rioba akiziona zile Makala zake Raia Mwema anaweza akazikana kabisa kuwa hakuwa yeye.
 
Hata kama wamelipia ila hoja ni kuwa tu kwa heshima aliyojijengea hapo kabla angejiuzulu tu ili asizidi kuuharibu Usomi wake.

TBC haikuwa hadhi yake, yeye angeenlea tu kufundisha.

Toka alivyopata huo ulaji Makala akawa ahandiki tena na hata mitandaoni akapotea kabisa. Hii inaitwa Ukitaka Mwafrika asahau kila kitu alichokuwa anapigania hapo awali basi mpe cheo.

Rioba akioziona zile Makala zake Raia Mwema anaweza akazikana kabisa kuwa hakuwa yeye.

Najiuliza akikutana na kina Jenerali now wanazungumza nini?
 
Hata pamoja na mambo yote lakini Rioba ameshindwa kuipandisha TBC angalau iwe nusu ya ile ya Tido ...basi tena ndio hivyo tusimlaumu
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom