TBC: Kongamano la watanzania waishio Marekani. Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Kabudi mgeni rasmi

master09

JF-Expert Member
Aug 12, 2013
808
559
Nipo naangalia TBC live sasa hivi, Prof.Kabudi anatoa nondo za hatari jinsi nchi ilipotoka na ilipo. Pia jinsi ilivyosaidia nchi nyingine kupata uhuru.

Mwaka 1980 Nyerere alinunua ndege mbili za ATC Kwa cash.Moja iliitwa Kilimanjaro na nyingine Serengeti Ila watu wanasahau amesisitiza.


MWITONGO MAARIFA anasema,
Kwann umeona busara kujibu swali linalohusu Tundu Lisu kupingwa risasi kwa lugha ya kiingereza? Katika kujibu kwa kiingereza pia uoni kwamba umeieleza dunia kwamba viongoz wetu hawana ulinzi?japo siamini Kama kwako Dodoma hapalindwi?

Kwann unasema watoto wako hawawezi kugombeA urais wa Tanzania?Nijuavyo wamezaliwa nje ya nchi na wewe baba yao ukiwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, je huo uraia wa kurithi wanaupataje? Sect 6 of citizenship act,1995...nazidi kuisoma tusiwanyime watoto wetu tuliozaa nje haki ya kuwa Marais wa nchi Yao

Uraia pacha umeujadili kwa zaidi ya nusu saa lakini umejikita kwenye fear of unknown, Ni upi msimamo wa Tanzania kwa diaspora Kama hatuna mpango na dual citizenship?Wanalindwa na sheria gani?Kama hakuna sheria tulitegemea uje ukiwa umejadili na serikali na mmeafikiana nn lakini naona hukuja kuzungumza na diaspora ukiwa na way foward au government stand...

Sijakusikia ukieleza nn Tanzania inategemea kutoka kwa diaspora


Hakuna inayomlinda mwanaume wa kigeni aliyeoa Mtanzania, wewe umesema wana privileges je Ni zipi?Mgeni akioa mtanzania haimpunguzii kulipa vibali Kama wageni wengine na tunao washkaji wanalipishwa..

Hayo Ni baadhi.....
 
Moja iliitwa Kilimanjaro na nyingine Serengeti Ila watu wanasahau. Kabudi yuko mubashara TBC akiunguruma kutokea Marekani akiwahutubia Diaspora
 
Nimemuona Dr. Ayoub Rioba akizungumza! nimetafakari mengi sana kwa jinsi nilivyomfahamu na yale maneno aliyotoa leo?anyway! ukurugenzi mtamu, ila siasa za nchi hii zinawadhalilisha sana wasomi wetu
Tupe habari
 
Kumbe Tabia ya Cash Purchase braza kairithi toka Kwa Mchonga
Usilinganishe Kilimanjaro na kichuguu!Mtu aliyeshindwa kulea watoto wake akihangaikia watanzania na Africa.Kwa kipindi chake na vipao mbele vya nchi wakati huo inawezekana alikuwa sahihi. Hakuna braza wako anachofanana na mchonga. Mchonga atabakia kuwa yeye Tz mpaka mwisho wa Dunia.
 
Nipo naangalia tbs live sasa hivi aisee prof.paramagamba anatoa nondo za hatari ...jinsi inchi ilipotoka nailipo, pia jinsi ilivyo saidia nnchi nyingine kupata uhuru ..


Sent using Jamii Forums mobile app
Hana chochote anachokisema. Katika watu hua siwaelewi ni huyu mzee.

Kwanza anaongea kama mwanaharakati anahamasisha jambo flani. Nani asiejua tulikua tunatawaliwa na uingereza na ujerumani huko nyuma, nani asiejua kua Nyerere alikua rais wa kwanza, nani asiejua kua tulipigana vita na Uganda, hadith kama hizo kuwaambia watu wazima ni ishara ya kuwadharau, hayo waambiwe watoto wadogo.

Pili hizo hadithi au historia za zamani zinatusaidia nini sisi? Zina msaada gani kwa Tanzania ya leo?

Mambo ya hovyo kabisa.
 
Usilinganishe Kilimanjaro na kichuguu!Mtu aliyeshindwa kulea watoto wake akihangaikia watanzania na Africa.Kwa kipindi chake na vipao mbele vya nchi wakati huo inawezekana alikuwa sahihi. Hakuna braza wako anachofanana na mchonga. Mchonga atabakia kuwa yeye Tz mpaka mwisho wa Dunia.

Mawazo yako Sio kanuni au sheria

Magu atafanya Makubwa Kuliko Nyerere
 
Back
Top Bottom