TBC international uozo mtupu

MIGUGO

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
2,136
3,924
TBC international 95.3 fm dsm ni Radio station ambayo sioni umuhimu wake.Nasema uozo kwa mambo yafuatayo niliyonotice:

1.Watangazaji hawajui kuongea kiingereza kwa ufasaha.Akiongea unamuonea huruma Kama atakosea labda.Ni kile cha kuungaunga.

2.Sauti kupungua na kuongezeka ghafla.Au kuwa kimya ghafla kwa mida hata dakika 3-5.

3.Muingiliano wa maongezi Na muziki.

4.Hawana dj mwenye ujuzi.Sijui wanaweka playlist ya computer Na kuondoka zao?

5.Inaingiza vipi mapato wakati haina matangazo ya biashara?

Mimi naona bora watumie kurusha bunge Na mambo muhimu ya Taifa Kama kutangaza Vivutio vya Asili Na kukaribisha wawekezaji kuliko kupiga miziki hasa ya mataifa ya magharibi.

Au wadau mnalionaje?
 
Tangu walipokubali kuwa station ya CCM wamekufa jumla, uoga umefanya washindwe kuwa wabunifu.
 
MBONA ni ya siku nyingi? WEAK METAL WILL BE REPLACED BY A SRONG METAL,kama kuna udhaifu wa kuongea kiingereza watakuja wanaoongea vizuri kwa kuwa nia ni kufanya vizuri zaidi ya hapo.
 
Tangu walipokubali kuwa station ya ccm wamekufa jumla, uoga umefanya washindwe kuwa wabunifu.

Radio ya sisiemu ni Uhuru fm.Salamu zimfikie mheshimiwa Nape Nauye.
 
MBONA ni ya siku nyingi? WEAK METAL WILL BE REPLACED BY A SRONG METAL,kama kuna udhaifu wa kuongea kiingereza watakuja wanaoongea vizuri kwa kuwa nia ni kufanya vizuri zaidi ya hapo.

Sio kiingereza Tu hapana hata uendeshwaji wa vipindi Na upendeleo wa kupiga nyimbo za magharibi.

SABC ya Africa Kusini 11/5/2016 ilitangaza kupiga miziki ya kwao 90%.

TBC ndio chombo pekee cha kuitangaza Tanzania.Kuwa ya kimataifa haimaanishi iwe ya kiingereza masaa 24.Basi tungekuwa Na vipindi vya kufundisha Kiswahili.Mfano Swahili to English,Swahili to Chinese,Swahili to Nyarwanda n.k.
 
Hivi kumbe bado kuna watu wanasikiliza TBC, mimi nilikuwa naangaliaga TBC1 kwa sababu ya bunge live, walipoacha kuonyesha bunge live ndiyo ukawa mwisho wangu wa kuangalia au kusikiliza TBC
 
SHIRIKA hili ni wakati sasa wa kujitanua zaidi kuwa na vituo vingi vya redio na tv vyenye kutumia teknolojiia ya kisasa ya mawasiliano ya habari kama yalivyo mashirika ya kitaifa ya nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom