TBC International Radio badilikeni

Ntemii

JF-Expert Member
May 25, 2022
289
519
Mimi ni mmoja wawasikilizaji wa redio hii kwa muda mrefu..kwakuwa nimetokea kukosa vipindi vizuri vya kuelimisha na kuongeza maarifa kutoka katika redio nyingi hapa mjini kwa kuwa nyingi zimejaa makanjanja wa mjini wenye uwezo mdogo wa kung'amua mambo..hivyo kuendekeza umbea na uchawa na taarabu.

Nikaona ni vyema nihamie kusikiliza Radio ya TBC International kusema ukweli pamoja na kuwa na vipindi vizuri vya kuelimisha hasa vya kidiplomasia na uchumi nawapongeza sana kwa hilo.

Ila shida moja tu vipindi vya namna hiyo ni vichache sana havizidi vitatu kwa siku nzima..baada ya hapo ni mziki mwanzo mwisho asubuhi mpka asubuhi.

Mbaya zaidi wanatumia playlist moja hiyo hiyo kila siku nyimbo zile zile hadi nimesha zikariri na kujua ipi inafata baada ya moja kuisha.

Hivyo basi naomba muongeze vipindi vya kiuchumi..biashara..diplomasia..mahusiano..kilomo na ufugaji..utunzaji wa mazingira n.k.

Mungu awabariki sana.
 
Back
Top Bottom