TBC iandae mahojiana kwa Wapinzani Pia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBC iandae mahojiana kwa Wapinzani Pia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Sep 11, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Katika Nchi ambazo zinafanya demokrasia ya Kweli na siyo ya kuigiza kama ilivyo kwa Tanzania, kwa hakika baada ya hotuba ya Rais, Tiddo Muhando angebidi awaweke Mwanasiasa wa Upinzania hata japo la Wataalamu wa masuala Mbalimbali katika Tanzania na Kuanza kujadili au kujibu hoja mbalimbali za Rais,

  Kwa hakika kwa kufanya hivyo Tanzania yote au Watanzania wanaweza kupata picha halisi au maelezo halisi toka wa kada mbalimbali katika kutokana nna hotuba ya Rais aliyeitoa kwa mwananchi kwa kuuliza maswali. TBC, Taifa inafaa washauriwe kuwa TBC ni mali ya Watanzania wote bila kujali Dini, Itikadi ya kisiasa ya Chama chochote kile, Kwa watu kama vyama vya upinzania nao inafaa kusikiliza mawazo yao katika hili na kutoa comments zao iwe CHADEMA, CUF, TLP, TADEA DP, TBC ni mali yao na tena inalipiwa kodi za Taifa la Tanzania. Rais wetu alifanya mahojiano moja kwa moja toka kwa Watanzania, hivyo kufanya kupata picha kwa upande mmoja. Kila Mtanzania anayo haki ya kupewa habari, na kutoa habari. Jaribu kutazama mahojiano ya Fox news, ABC, CCN International, CCN News, BBC, VOA, utaona kwa kiasi gani kama usawa unakuapo katika Habari. Tanzania ni ya kwetu wote bila ya kujali itikadi wa Chama cha siasa.
   
 2. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Juu ya kutafuta critics nakubaliana nawe na hilo ni performance level ya vyombo vyetu - hatuna analysts wanaoalikwaga/consulted kuongelea haya mambo; angalau akina ITV wanajitahidi na vipima joto etc.

  Ila hilo la kuwaita viongozi wa upinzani kufanya the same sidhani kama ni sahihi maana Kikwete aliongea kama Rais na sio kama mwana CCM. Ni ngumu kuepuka kuongelea siasa in such a discussion because ilani ya CCM ndiyo inayotekelezwa. Sema tu mambo specific ya CCM hayakutakiwa kuwa kwenye ule mjadala.
   
 3. k

  kigugumizi Member

  #3
  Sep 11, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wazo hilo.
  Vyama vya upinzani ni jicho la pili la jamii, lenye kukosoa, kushauri na kujenga, inabidi Tido Mhando aweze kuwaita viongozi wa vyama vya upinzani - Chadema na Cuf ambavyo vipi serious ili viweze kutoa ufafanuzi mbadala kama Vyama mbadala kwa Taifa hili.

  Sidhani kama Tido Mhando anaweza kufanya hayo!! Nasikia kipindi kilirekodiwa?? Eti kweli? Ni taarifa za ndani kutoka kwa mtu wa ndani wa TBC!! Jaribuni kufatilia vyema!!
   
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mbona robo ya maongezi yalijaa majibu ya chama Chao cha CCM, "Hivi mbona CCM ina makundi" haya sio mambo ya kuongelea katika Taifa labda kwenye vikao vya Chama Je na Sisi tusio kuwa na Chama itakuaje?? Haya masuala ya kuchukiana kwa wabunge wa CCM ni waongee ndani ya vikao vyao, na watoe matamko nje ya Taifa lote
   
 5. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Duh kama ndio hivyo basi itakuwa ni aibu ile mbaya, tutajaribu kufanya hivyo
   
 6. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kigugumizi,

  Sitegemei kwa hilo nadhani ni uzushi huo, mbona ilikuwa LIVE kwenye vyombo vingi vya habari!! Nadhani kabla ya kupost kitu kama hiki tuwe kwanza tunakuwa na uhakika, ukiona huna hakika achana nacho.

  Kuhusu TBC iandae mahojiano na wapinzani sitegemei kama TBC wanaweza kufanya hiyo kama wanafikia hata kuwazimia wapinzani wakiwa kwenye bunge wakihofia usalama wa nchi!

  Pia hii imemjenga JK nadhani ilikuwa imechanganywa na kampeni humo humo alivyoanza kuelezea mambo ya barabara za Kigoma/Bukoba n.k tiyari alikuwa kwenye mambo ya Ilani ya CCM, kwahiyo TBC hawawezi kukubali kumbomoa kupitia wapinzani. Ni maoni yangu haya.
   
 7. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata kama si kweli lakini dalili zote zinaonyesha hivyo. Impossible kuwatangazia wananchi namba zoote zile za simu halafu ushindwe kupokea hata simu tano tu? wehu gani huo

  Halafu maswali yalikaakaa kama vile yalipangwa hata majibu yake yalikuwa na data nyingi mno bila hata ya reference. Siamini raisi huyu anayajua matatizo ya nchi hii kiundani hivyo maana yangemsuta ayatafutie majibu. Najfikiri aliyakremisha akifikiri atafurahisha umma. Vijiji vya huko ndani Kigoma, Mtwara na Lindi na urefu wa barabara fulani anekumbukaje vyote hivyo? Idadi ya walimu wasiolipwa na exact amount! Mtu makini ndio anatakiwa ajue vyote hivyo by heart maana anavishughulikia. Kwa yeye siamini! Alikesha wiki nzima aki train hiyo movie.
   
 8. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kulikuwa hakuna takwimu kama kipindi cha Mkapa, lakini yeye mara nyingi huwa naseema yale mambo anayoyajua yeye
   
 9. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sasa Watanzania at least wanaanza kuelewa Viongozi wao wapo vipi na tabia zao
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Haiwezekani kwa wapinzani ,sasa utawaulizaje wapinzani wakati Serikali inaendeshwa na Chama kingine,muendelezo uwe kwa masuali mafupi ambayo yatahitaji maelezo kutoka kwa wakuu walioko serikalini na idara zake ,sasa inakuwaje mtu anahitaji umeme anaambiwa akanunue maguzo na waya za umeme na pia awalipe mafundi ,suali kama hilo ndilo masuala ambayo yanafaa kuulizwa wahusika ,saa mpinzani utamuulizaje ,hapa mpinzani hana nafasi ya kujibu na hahusiki kabisa kwani si wakati wake.
   
 11. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Watatoa mawazo mbadala kwa jamii yote na pia kuona kama jamii yote inapewa hali swa kwa wote wote
   
 12. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Vyama vya upinzania ni serikali mbadala kwa kuwa na kazi moja na nayo huwa wanaongoza serikali, sasa lazima ujue kuwa mfumo wa vyama vingi kazi yake ni nini
   
 13. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2009
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa uk nimeona pindi Brawn anapomaliza kuhojiwa iwe kwa lolote lile basi basi Cameronnaye atapewajapo sekunde kuelezea/au kufafanua ambacho waziri mkuu amekisema......so ni vyema kuwapa wapinzani kajinafasi hata kajisekunde.
   
 14. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sasa tunafuta Demokrasia ya mambo ya kuigiza tu, maana katika demokrasia ya kweli lazima watu wa pande zote kutoa mawazo yao yote
   
Loading...