TBC hongera kwa hili

julaibibi

JF-Expert Member
Jun 16, 2020
1,485
2,000
Kuna hii ziara ya bandarini aliyoifanya mzee na benki kuu makala mnairusha aise inanikosha sana.

Ziara ya pale bandarin hasa pale mzee amewabana wale jamaa wa kuscan mizigo aisee kweli pale aliwabana maana inaonesha tayari mzee alikua ana info za kutosha alifika kujiridhisha.

Nashauri sana huu utaratibu wa kuweka vijana kila mahali wawe wanatoa taarifa za utendaji. Yaani kuwe na chawa kila mahali hio ndio mbinu nzuri watu wafanye kazi.

Aise jamaa walichanganyikiwa wanamueleza sijui container hatuwez kujua vilivyomo sijui mpaka vifanyaje sijui mpaka viifanyaje.

TBC makala hizi zinazipa uchungu sana kuona namna gani jembe letu lilivopiga kazi jamani.

Kwa uelekeo huu, ziara za ghafla ziwe ndio chachu na pamoja na kuzifatilia hela hukohuko walipozila wazitolee matundu yote waliyoingizia.
 

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
1,882
2,000
Mkuu,Unaelewa kinachofanyika katika scanners za Mizigo? Umewahi kufika Airport au Bandarani? Kuscan Mzigo ni hatua moja,Kuanalyse picha ni hatua nyingine.Kwa mzigo ambao uko kwenye kontena kubwa ni zoezi pevu sana ambalo ni la kitaalamu linatumia mfumo wa rangi ambazo kila rangi huwa na tafsiri yake.

Usione wale walikuwa wanashindwa kumuelekeza ni kwa sababu ile process sio ya dakika moja bali ni ya muda.Anyway kwa sababu lengo lilikuwa ni kuonesha kuwa kuna upigaji ilibidi mazingira yawekwe katika hali ile.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom