TBC haya ni majanga

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,674
1,685
Naangalia sherehe za uhuru wa Tanganyika kupitia TBC. Kilicho nifadhaisha ni kumsikia mtangazaji wa kiume akisema TAA ni Tanzania African Association. Ninavofahamu mie kirefu chake ni Tanganyika African Association.
 
Ni Stanley Ganzel huyu anashindwa na mdada Anna Mwasyoke ambaye yeye anatamka wazi na sahihi kuwa leo ni kuadhimisha uhuru wa TANGANYIKA.
 
kwani wewe upo wap mkuu?

Hapahapa Bongo, na hakuna ubishi kuwa hii ni nchi ya vilaza, inaongozwa na vilaza, vitengo vimeshikwa na vilaza, ukiona system ya elimu inaongozwa na vilaza basi utegemee mazao ya vilaza, enzi za mwalimu haiku hivi! Sijui tumerogwa...makanjanja mpaka wanashika wizara...aaaaaaaaargh!:frusty:
 
Ni Stanley Ganzel huyu anashindwa na mdada Anna Mwasyoke ambaye yeye anatamka wazi na sahihi kuwa leo ni kuadhimisha uhuru wa TANGANYIKA.

Bora hata Ganzel kidogo, kuna jamaa anaitwa Marin Hassan sijui kasomea wapi huyu maskini wa mungu, au ndy ukiwa kibaraka sharti ujitoe akili!
 
Huyu, bolded, katokea TVZ (Television Zanzibar) siku hizi ZBC (Zanzibar Broadcasting Corporation.
 
Naangalia sherehe za uhuru wa Tanganyika kupitia TBC. Kilicho nifadhaisha ni kumsikia mtangazaji wa kiume akisema TAA ni Tanzania African Association. Ninavofahamu mie kirefu chake ni Tanganyika African Association.
Huyo Mtangazaji leo kasema UONGO ULIOKITHIRI SANA kiasi cha kwamba uongozi wa TBC unatakiwa uombe radhi kwa WaTZ. Kwa mfano amesema "Nyerere alianzisha jeshi la mgambo kiasi cha miaka ya sitini ili watu wote wapitie mgambo baadaye akilibadilisha likawa ni Jeshi la Kujenga Taifa".
 
Mkuu, yaonekana hapo TBC wasema UKWELI na UHAKIKA siku hizi hawatakiwi na yawezekana kiazi huyu akapandishwa cheo.
 
Hii TBC mbona wanakata matangazo ama n hiki kitivi changu.
Hivi vipaumbele vyao ni vipi? Maana wanaweka mambo ya kipuuzi na kuacha kutuonesha mambo ya msingi KWETU.
 
Watanzania kwa lawama du! Acha kabisa wewe unayelalamika hapa inawezekana hata familia yako kuiongoza huwezi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom