TBC hamna jipya: huku uzinduzi wa studio, huku msafara wa rais, lakini Bunge live hamtaki

Mr. Hussein Juma

Verified Member
Mar 5, 2012
729
1,000
Yaani huwa nikifikiria Tanzania ya viwanda inavyoendeshwa, ni kama nchi ya mazuzu wote. Leo TBC wanazindua studio huko Arusha na huku Chato, mheshimiwa rais anatoka ziarani Chato kuelekea Singida.

Basi mbwembwe haziishi, mara matangazo yahamie Arusha, mara yahamie kwenye msafara wa rais...yaani ni fujo tupu. Hivi hizi mbwembwe kwa nini zisingehamishiwa kwenye juhudi za kuonesha Bunge mubashara ili watu wanufaike na mijadala ya maendeleo kwa wananchi.

Hizi mbwembwe zenu TBC hazina maana hata kidogo kama watu wanaishi kama mashetani, binafsi mimi hizi naziita 'kiki' kama kiki zingine. TBC hamna jipya, yaani hamna cha maana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom