Kumbukumbuyatorati
Senior Member
- Jul 27, 2018
- 152
- 220
TBC1 mnatia aibu sana. Hii si sawa kabisa. Kama ni maagizo "kutoka juu" basi tujue tunapotoka katika dhana ya utawala bora katika tasnia ya habari. Inasikitisha sana maana tunajenga uhasama katika jamii. Laiti mngeingia ndani ya moyo na fikra zangu ninavyotamani umoja, mshikamano na Utaifa wetu msingefanya hivi.
Hivi kweli Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na Mbunge wake Esther Matiko wamekaa ndani takriban miezi mitati Leo wameachiwa huru kweli hii si habari basi hata ya mwisho? Kwamba Mbowe na Matiko si habari ya kuwaambia Watanzania? Kweli?
Hivi tunajua TBC ni chombo cha umma! Tunajua hata wale wafuasi wa CHADEMA nao wanalipa kodi inayoendesha TBC? Kweli? Mkurugenzi Dk. Ayubu Ryoba kweli habari zote Tanzania hii kwenu si habari?