TBC haitendi haki sawa kwa vyama vyote vya siasa

Mtabe

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
675
96
Ndugu wana J-Forum napenda kuleta jamvini suala moja ambalo linanikera sana. Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu habari za kituo cha TV ya Taifa TBC imekuwa ikitoa habari kwa kupendelea chama cha mapinduzi kwa kurusha ktk taarifa za habari chaguzi zake mbalimbaali ndani ya chama sehemu mbalimbali za nchi. Kitu cha kushangaza ni kwamba Operesheni za vuguvugu la mabadiliko al maarufu kama M4C zinazoendeshwa na CHADEMA maeneo mbalimbali ya nchi au kampeni za udiwani ktk kata mbalimbali hazionyeshwi hata clip ya nusu dakika hiki ni kitu cha kushangaza sana. Je, kituo hiki ni cha CCM au ni cha Umma? Naomba kuwasilisha!!!!!
 
TV hovyo hovyo haina integrity. Achana nao hao, tutaajiri ma-professional January 2016.
 
Mimi nilisha sahau kama kuna TV inaitwa TBC hapa nchini, kwasababu hii Tv ipo kiCCM Zaidi badala ya kuwa ya TAIFA
.By oremus
 
Haingii akilini hata kidogo, hata kama wao ndo wenye nchi at least waonyesha fairness ili tujue wanaunga mkono kukuwa kwa demokrasia nchini. Chombo cha habari cha UMMA kinapaswa kuonyesha habari bila upendeleo wowote.
 
Wana akili hiyo? wamejaa ubinafsi na uroho wa madaraka.
 
Wengine huwa tunaangaliaga hii TV kipindi cha Original Comedy tu, mke wangu yeye hupenda kuangalia na kipindi chao cha Chereko basi, vinginevyo hii sio chanzo changu habari kabisa, ningependa wazalendo wengine wengi tuungane mkono katika hili.
 
TV hovyo hovyo haina integrity. Achana nao hao, tutaajiri ma-professional January 2016.

issue sio waajiriwa, au wakurugenzi. ni sera za chombo. hata chadema wakiingia they would like to have a lion share of coverage
 
issue sio waajiriwa, au wakurugenzi. ni sera za chombo. hata chadema wakiingia they would like to have a lion share of coverage
Inategemea na kiongozi, hawa wa BMW hawawezi kuiboresha policy. Kwanza CEO ndie anayependekeza maboresho ya policy kwa board, hatujawahi kusikia hii kitu, ndio maana nazungumzia uongozi (Mkurugenzi) Vs professionalism. Angalia sasa gazeti la mwanahalisi limefungiwa, je press conference yake, ina tofauti gani na context ya mwanahalisi. Hata JF leo wanaogopa kuweka context za press conference. Wakurugenzi wanajikomba kwa sababu wanahongwa vyeo. Tido angeweza, umeona kilichotokea. January 2016 itashughulikiwa.
 
Ndio maana tumeamua kwamba tukishang'oa ccm mambo ya awali tutakaofanya ni pamoja na kuifuta kabisa TBC , na majengo yake tutayageuza soko , huku tukitimua wafanyakazi wake wote akiwemo Mkurugenzi wake , kuanza upya si ujinga .
interesting khaaaa
lini hyo mtaing'oa hyo ccm?
 
Mi sioni kabisa tbc ikifanya kazi kama chombo cha umma yaani publi good ambapo huwa public good ina sifa nne
1. Non exccludable
2. Non rivarly
3. Free rider problem
4. Non divible
5. Zero marginal coss
Sasa naona hizo sifa zote kwa tbc hazipo kwano ni so much excludable nk
HAMA HUKO ULIKO UTAJUA YOOTE
 
Hao TBC hawajielewi, wakati chombo hicho kinaendeshwa kwa kodi zetu sote bila kujali itikadi zetu za kisiasa, Nina maana kinaendeshwa kwa kodi za wanaccm na wasio wanaccm

Lakini jinsi kinavyoendeshwa kwa propaganda za kukisaidia chama tawala cha CCM ni heri tu kingekuwa kinaendeshwa kwa michango ya wanaccm pekee
 
Back
Top Bottom