Tbc enzi hizo na safari za kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tbc enzi hizo na safari za kikwete

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ground Zero, Jul 20, 2011.

 1. Ground Zero

  Ground Zero JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana jf. Mimi si mchangiaji wa mara kwa mara lakini leo nataka niseme hili kwa kile ambacho nadhani ni mkakati wa kuhalalisha safari za raisi wetu nje ya nchi.

  Kwa kutumia kipindi chake cha enzi hizo, TBC imekuwa ikituonesha safari zilizokuwa zikifanywa na baba wa taifa nje ya nchi bila kutuonesha alichokizungumza au madhumuni ya safari. TBC inaonekana kuwa interested na matukio zaidi badala ya dhima ya safari yenyewe. Kinachonishangaza zaidi ni kwamba wanaweza wakarudia safari ya nchi moja mara nyingi nadhani ili tuamini kuwa naye mwalimu alikuwa anasafiri sana. TBC tuonesheni picha za mwalimu akisaidiana na wakulima na wafanyakazi vijijini kujenga,kulima na sio mtuoneshe safari za Nigeria kila siku.

  Msipofanya hivyo tutaamini mnatumia safari za mwalimu kuhalalisha safari za Kikwete.UHURU NA KAZI!
   
 2. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Nafikiri wanataka tuseme Mbona Nyerere alikuwa anasafiri sana, Nyerere hajawahi kusafiri akaacha nchi ina matatizo na kukwea pipa kama huyu Zee la Anga a.k.a Vasco Da Gama II wa Tanzania
   
 3. K

  KAPIRIPIRI Member

  #3
  Jul 20, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Baada ya kufatilia kipindi hiki nimejiuliza maswali mawilli
  1.Kwanini safari zile zile wamekuwa wakizirudia mara kwa mara?
  2.Mbona tunaoneshwa picha tu na hatusikii alichokisema kwenye ziara hizo?
  Anyway? walau nilichobaini ni kuwa kama huu ndo mpango wao wa kuhararisha UZURURULAJI wa rais wetu basi wameenda chaka.Leo nimesikitishwa na kauli za mheshimiwa wetu kupitia BBC Idhaa ya Kiswahill anasema eti ameenda Afrika Kusini kuihuza Tz kibiashara yaani kutafuta wawekezaji.Nina maswali mawili kwake
  1.Hivi hii nchi inayochuuzwa kiholela si kuna siku itauzwa hata kwa maharamia?
  2.Nini bora zaidi, kwanza kubaki nchini na kutatua kwanza tatizo la umeme kwa suluhu la kudumu au kuendelea kutafuta watu ili wawekeze gizani?
  Jamani Tz tutaondokana lini na KIPINDUPINDU cha fikra?
   
 4. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Wtz tuna tatizo la ukosefu wa rais nchini (URN:) pamoja na na kwamba siruhusiwi kuongea vibaya juu ni rais ya leo ni kali kuliko. Maana rais amedhirisha uwezo wake ni mdogo kwa sababu anadhani hata dunia ina wavivu wa kufilia kama watz.Ametaka dunia ielewe kwamba tatizo la umeme tz ni ukame.Tatizo sio hilo daktar jk tatizo ni ccm na watu wake.Kama ni ukame hata kwa nchi jirani hata nchi nyingine zingekuwa na tatizo hilo hilo
   
Loading...