Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
TBC ni Televisheni ya Taifa na inaendeshwa kwa kodi za wananchi wote, bila kujali itikadi zao za kisiasa
Kutokana na hali hiyo ni LAZIMA, TBC iendeshwe kwa matakwa ya walipa kodi wa nchi hii, ambao ndiyo wanaifanya iendekee ku-survive
Kwa Televisheni yetu ya Taifa inavyoendeshwa, ni kama Mali binafsi ya Magufuli, Rais wa nchi hii.
Nitatoa mfano ninachomaanisha
Wakati awamu ya tano ilipoingia madarakani, walifuta kuonyesha Live, matangazo ya Bunge, kwa sababu za "kipuuzi" eti hawawezi kuonyesha Live matangazo hayo, kwa kuwa huo ni muda wa kazi na awamu hii imejitanabaisha kwa slogan yake HAPA KAZI TU
Kama kweli TBC ingekuwa Televisheni ya Taifa, ingesikiliza maoni ya watanzania namna wanavyotaka Televisheni hiyo ya Taifa, namna gani wanataka iendeshwe
Nakumbuka wakati yanafutwa matangazo hayo mubashara, wabunge wa upinzani na wananchi wenyewe walipa kodi inayoendesha Televisheni hiyo, walipinga vikali, kufuta matangazo hayo ya moja kwa moja
Hata hivyo tulichojionea baada ya kufutwa matangazo hayo, ni kila tukio linalotokea Ikulu, kuanzia kuapishwa kwa wateule wake, kukutana na vikundi mbalimbali vya kijamii, yakirushwa moja kwa moja mubashara na Televisheni hiyo na kitu kinachoshangaza ni kuwa matukio yote hayo yanatokea majira ya kufanya kazi, majira ambayo tuliambiwa watanzania kuwa majira ya kazi, kwa hiyo watanzania hatupaswi kuangalia Televisheni na badala yake tunatakiwa tuchape kazi, kwa kuwa slogan ya awamu ya tano ya serikali ni HAPA KAZI TUU!
Hata hivyo Bahati nzuri katika moja ya hotuba zake, Mheshimiwa Rais alikiri mwenyewe kuwa ni yeye aliyefuta matangazo hayo mubashara ya Bunge, kwa "kuwaagiza" wabunge wake wa CCM kwa kutumia uwingi wao kuyafuta matangazo hayo ya moja kwa moja!
Kitu kinachoniuma zaidi ni hili tukio la hivi sasa la michuano ya AFCON inayoendelea nchini Misri kipindi hiki, ambapo timu yetu ya Taifa imefuzu kwenye fainali hizo
Habari za uhakika ni kuwa timu zote zilizofuzu fainali ya michuano hiyo, Televisheni za nchi zao, zinaonyesha mubashara michuano hiyo, ikiwemo jirani zetu Kenya na kutufanya sisi kuwa ni nchi pekee, kati ya nchi zilizofuzu kwenye fainali hizo kutoonyesha michuano hiyo mubashara!
Ningependa kuwauliza manejimenti ya TBC, je Televisheni hiyo inaendeshwa kwa matakwa ya walipa kodi wa nchi hii, ambao ndiyo wananchi, wanayoifanya Televisheni hiyo Iendelee ku-survive au ni kutokana na matakwa ya Mkuu wa nchi hii??