TBC acheni kumuelekeza Mama Samia njia ya kupita

Tee Bag

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
7,200
5,553
Nyie "Tibisii" nisikilizeni niwasaidie. Acheni kumuelekeza Mama Samia njia ya kupita. Hoja zenu kila siku ni "mama Samia avae viatu vya Magufuli, mama Samia apite njia ya Magufuli, mama Samia aendeleze yale aliyoacha Magufuli, mama Samia ajipime kwa viatu vya Magufuli, mama Samia alikua mwanafunzi mzuri wa Magufuli, mama Samia amalizie kazi aliyoacha Magufuli"

Muacheni MAMA afanye vile atakavyoona inafaa, ili mradi iwe kwa maslahi ya taifa letu. Yale mazuri aliyofanya Rais Magufuli tutayaenzi, lakini tusimlazimishe Mama Samia apite njia ileile ya Magufuli au afanye yaleyale.

Kumbukeni huyu sio msaidizi tena wa Magufuli. Huyu ni Rais wa nchi mwenye mamlaka kamili. Ana haki ya kuchagua njia yake anayoona inafaa kusaidia nchi. Msimlazimishe kuendeleza 'legacy' ya Magufuli. Ana haki ya kutengeneza 'legacy" yake kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo. Tumeelewana nadhani. Zindukeni kabla hamjazinduliwa!


FB_IMG_1617037473080.jpg
 
Sasa hutaki? Watz ndiyo wanavyosema.. wewe nani kwenye serikali mpaka uwazuie TBC1 kutangaza mawazo ya watz waliowengi?
WaTZ gani hao?? Sema wewe unavyosema!! Tibisiii waache udwanzi....Yaani wanataka Mama samia apite njia ya magufuli ya kuokota watu kwenye viroba? Apitie njia ya watu wasiojulikana?

Apitie kuwatowapandisha wafanyakazi mishahara? Apitie njia ya kuzuia watu wasichukue mafao yao pindi ajira ikikoma? Apitie kuipa tenda kampuni zake binafsi? Apitie kufanya mambo bila kufuata katiba au taratibu? Apitie ...Apitieee...Apitiieeeeee!!
 
Unasema “Kumbukeni huyu sio msaidizi tena wa Magufuli. Huyu ni Rais wa nchi mwenye mamlaka kamili”.

Watamlazimisha vipi wakati ni Rais Mwenye mamlaka kamili?

Yaani unaweza kumlazimisha Rais wa Tanzania kufanya kitu unachokitaka?

Hoja zako zinakinzana kihoja na ukweli!

Ndio maana kamalizia zindukeni kanla hamjazinduliwa. Maana mama ni mtaratibu ila wasipokuwa makini ita backfire muda si mrefu
 
WaTZ gani hao?? Sema wewe unavyosema!! Tibisiii waache udwanzi....Yaani wanataka Mama samia apite njia ya magufuli ya kuokota watu kwenye viroba? Apitie njia ya watu wasiojulikana? Apitie kuwatowapandisha wafanyakazi mishahara? Apitie njia ya kuzuia watu wasichukue mafao yao pindi ajira ikikoma? Apitie kuipa tenda kampuni zake binafsi? Apitie kufanya mambo bila kufuata katiba au taratibu? Apitie ...Apitieee...Apitiieeeeee!!
Sasa wewe unawasemea watz wapi? Mimi nawasemea watz hawa kwenye video clip hizi hapa



 
WaTZ gani hao?? Sema wewe unavyosema!! Tibisiii waache udwanzi....Yaani wanataka Mama samia apite njia ya magufuli ya kuokota watu kwenye viroba? Apitie njia ya watu wasiojulikana? Apitie kuwatowapandisha wafanyakazi mishahara? Apitie njia ya kuzuia watu wasichukue mafao yao pindi ajira ikikoma? Apitie kuipa tenda kampuni zake binafsi? Apitie kufanya mambo bila kufuata katiba au taratibu? Apitie ...Apitieee...Apitiieeeeee!!
Tuombe Mungu atuepushe kupita njia hizo manake unaewa tamani kujotoa mhanga ili uondoke na mtu
 
Back
Top Bottom